Jumatatu 22 Juni 2026 - 22:17
Mpango wa Kuuangamiza Muqawama na Hizbullah Umeshindwa

Hawza/ Sheikh Naim Qassim, Katibu Mkuu wa Hizbullah, amesema kuwa; kulikuwa na mpango wa kuiangamiza Hizbullah na Muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati, lakini mpango huo umeshindwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Naim Qassim, Katibu Mkuu wa Hizbullah, amesema kuwa; kulikuwa na mpango wa kuiangamiza Hizbullah na Muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati, lakini mpango huo umefeli,  wakati wa operesheni ya “Asf Ma'kul” nchini Lebanon, karibu mashambulizi 10,000 ya anga yalifanyika, lakini licha ya kujitolea huku kote, Muqawama umeendelea kusimama imara. Mpango wa kuiangamiza Iran na Muqawama katika eneo hili ulishindwa, na kwa hiyo hatua mpya imeanza ambayo matokeo yake ni kushindwa kwa mpango wa Marekani na Israel.

Sheikh Naim Qassim, Katibu Mkuu wa Hizbullah, alisema kuwa; uchokozi wa Israel umeshindwa na haukuweza kufikia malengo yake, lakini Waisraeli bado wana matumaini ya kubadilisha hali ya mambo.

Iran, licha ya kujitolea kwake kwa kiwango kikubwa na cha kipekee, imejitokeza ikiwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali na imethibitisha kuwa haitaachana na haki yake. Adui Muisraeli hakuzingatia makubaliano ya kusitisha uchokozi ya tarehe 27 Novemba 2024, na kupitia vita dhidi ya Iran, ilijaribu kuuangamiza mhimili mkuu wa Muqawama katika ulimwengu wa Kiarabu.

Sheikh Naim Qassim, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, alisema katika hotuba yake: “Usitishaji vita unaoambatana na uhuru wa Israel kufanya inavyotaka ni muendelezo wa uchokozi, na sisi hatuukubali.”

Hatukukubali mpango huu katika kipindi chote cha miezi 15 baada ya makubaliano ya tarehe 27 Novemba, kila mara tuliposhikamana na usitishaji vita, adui hakushikamana nahilo, sasa tuko katika hatua ya kuvunja mpango wa Israel, na usitishaji vita unamaanisha kusimamishwa kikamilifu kwa uchokozi kabla ya adui kuondoka katika ardhi yetu. Usitishaji vita maana yake ni kusimamishwa kabisa kwa mashambulizi ya anga, ardhini na baharini, kutofanyika uharibifu wowote, na kutotumwa vikosi vya ziada katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

Sheikh Naim Qassim, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, alisema: “Tunaona uungaji mkono mkubwa kutoka Iran, ambapo katika kipengele cha kwanza (cha makubaliano) iliweka wazi suala la kusimamisha uchokozi dhidi ya Lebanon na kuilinda nchi hiyo.”

Akiihutubia serikali ya Lebanon alisema: “Mazungumzo ya moja kwa moja na adui yameleta mafanikio gani zaidi ya kumpatia adui huyo upendeleo na nafasi zaidi? Itazameni Iran kubwa, ambayo iko tayari kufunga Mlango wa Hormuz kwa ajili ya Lebanon; hii ni silaha iliyopo mikononi mwenu, enyi serikali ya Lebanon.”

Sheikh Naim Qassim, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, alisema: “Uchokozi huu usingefikia kiwango hiki bila uungaji mkono wa Marekani; kwa hiyo Rais wa Marekani ana uwezo wa kuusimamisha uchokozi huo.”

Kubaki katika ardhi ya Lebanon haiwezekani, na chini ya kivuli cha uvamizi hakuna eneo lolote lililo salama, tunalo jeshi la taifa ambalo ndilo pekee lililoko ardhini na linalolinda mamlaka na uhuru wa nchi, nasi tunashirikiana nalo.

Sheikh Naim Qassim, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, alisema: “Nchini Lebanon hakuna kundi lolote litakalokuwa na ubora juu ya jingine, Lebanon inaweza kusimama na kuendelea tu kupitia kuishi pamoja na umoja.”

Ninaitaka serikali ambayo ina hamasa kubwa ya kumaliza uadui na adui, isiongeze uadui dhidi ya wananchi wa Lebanon. Ninampongeza Suleiman Frangieh, kiongozi wa Harakati ya Al-Marada, ambaye kutokana na kushikamana kwake na misingi na kanuni zake amewekwa katika orodha ya vikwazo vya Marekani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha