Jumatatu 22 Juni 2026 - 23:30
Israel Imethibitisha Mara Nyingi Kutoheshimu Makubaliano na Sheria za Kimataifa

Hawza/ Ali Ammar amesisitiza kwamba; mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya Lebanon na juhudi zake za kusonga mbele kuelekea eneo la “Ali al-Tahir” yanafanyika katika mfumo wa sera endelevu ya uchokozi.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Ali Ammar, mwanachama wa Kambi ya Uaminifu kwa Muqawama na Mbunge wa Lebanon, katika mahojiano yake na Redio Al-Risalah, alisisitiza kwamba; mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya Lebanon na jitihada za kusonga mbele kuelekea eneo la “Ali al-Tahir” yanafanyika katika mfumo wa mkabala wa uchokozi unaoendelea.

Akiweka mkazo kwamba; Israel imeonesha mara nyingi kutoheshimu makubaliano au sheria za kimataifa, alisema: “Kuweka matumaini au kutegemea makubaliano yoyote kati ya Marekani na Iran kunapaswa pia kuzingatia kiwango cha kujifunga kwa upande wa Israel katika kutekeleza makubaliano hayo.”

Ammar pia alieleza kuwa; kipengele kinachohusiana na kujiondoa kwa Israel ndani ya muda wa siku 60 bado kinategemea uwezo wa pande husika kuhakikisha utekelezaji wake.

Mwanachama huyo wa Kambi ya Muqawama, huku akirejelea jitihada za kusonga mbele kuelekea eneo la Ali al-Tahir, alisema kuwa; kwa mtazamo wa jeshi la uvamizi la Israel, eneo hilo lina umuhimu wa kiroho na wa kiishara, kwa kuwa katika mapambano yaliyopita lilikuwa alama muhimu na lilisababisha hasara kubwa za kibinadamu na kimali kwa vikosi vya uvamizi. Anaamini kwamba Israel inajaribu kufidia kushindwa kwake kupitia kupata mafanikio ya kiishara.

Ammar, kuhusu mjadala wa kile kinachoitwa “tofauti kati ya Marekani na Israel”, alisema: “Huenda hali hii isiwe tofauti ya kweli, bali ni mgawanyo wa majukumu ambapo kila upande una mahesabu yake maalumu ya kisiasa.”

Kuhusu msimamo wa Iran, alisisitiza kuwa; Iran imethibitisha kujifunga kwake katika kuunga mkono Muqawama na imekuwa pamoja nao tangu mwanzo wa njia hiyo, pia aliashiria uaminifu wa Iran katika kutekeleza ahadi na wajibu wake.

Mwishoni, mwanachama huyo wa Kambi ya Muqawama, akizungumzia uhusiano kati ya Harakati ya Amal na Hizbullah, alisisitiza kwamba; pande hizi mbili ni nyuso mbili za sarafu moja katika njia moja, alisema kuwa zinafanya kazi kwa mujibu wa mkabala wa Imam Musa al-Sadr na Imam Khomeini, jambo ambalo Mheshimiwa Nabih Berri, Spika wa Bunge la Lebanon, analidhihirisha kupitia mwenendo wake wa kiungwana na wenye athari katika kutafsiri na kutekeleza mwelekeo wa viongozi hao wawili kwa ajili ya kulinda mamlaka ya taifa na kutetea malengo ya wanaotafuta haki.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha