Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Qasim Hashim, Mbunge wa Lebanon na mwanachama wa Kambi ya “Maendeleo na Uhuru”, amesema kwamba; kuendelea kwa uchokozi wa Israel huku ulimwengu ukinyamaza kunathibitisha asili ya kiuchokozi ya utawala ambao kamwe haujawahi na hautawahi kujifunga na maazimio, sheria, mila na mikataba ya kimataifa, na ambao kila siku unakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu na kuvuka mipaka yake.
Aliongeza kusema: “Yale yaliyotokea tangu kutangazwa kwa hati ya maelewano kati ya Marekani na Iran hadi sasa, kuanzia mauaji na uharibifu hadi kupanuka kwa mashambulizi ya Israel, yanaziweka serikali husika katika maelewano hayo pamoja na wale wanaotoa dhamana na mwamvuli unaohitajika kwa ajili ya kuimarisha misingi ya uthabiti inaohitajika katika eneo hili na hata nje yake kwa kutegemea Lebanon, mbele ya jukumu kubwa na zito la kukomesha kiburi, uasi na uhalifu wa Kizayuni; uhalifu ambao sasa unatishia usalama na uthabiti wa kimataifa.”
Akasema kuwa; katika dunia inayojinasibu kwa haki na haki za binadamu, haifai kuficha uhalifu wa Israel wala kuwasafisha wahusika wake dhidi ya ukatili huu wa kinyama na kuwafanya kana kwamba hawana hatia.
Maoni yako