Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Shirika la Habari la Anadolu, kikao cha 114 cha Mkutano wa Kimataifa wa Kazi wa International Labour Organization kinaendelea kufanyika katika mji wa Geneva nchini Switzerland.
Katika kikao cha wazi, wakati wa kujadili suala lililohusiana na upigaji kura wa siku iliyotangulia, mwanadiplomasia wa Israel, Walid Gadban, hakufanikiwa kumaliza hotuba yake kutokana na radi amal na upinzani mkubwa kutoka kwa watu waliokuwepo ukumbini hapo.
Katika mkutano huo, mawaziri kadhaa kutoka nchi mbalimbali pamoja na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi na waajiri walionyesha upinzani wao kwa kugonga meza wakati afisa huyo wa Israel alipokuwa akizungumza.
Wakati wa upinzani huo, baadhi ya maafisa waliokuwapo ukumbini waliinua bendera za Palestina, lakini walipewa tahadhari na vikosi vya usalama na kuombwa kuzishusha bendera hizo.
Licha ya maonyo ya Juan Castillo, rais wa Mkutano wa 114 wa Kimataifa wa Kazi, upinzani uliendelea, hatimaye afisa huyo wa Israel alilazimika kuondoka kabla ya kumaliza hotuba yake, na nafasi ikatolewa kwa mzungumzaji aliyefuata.
Pia ilionekana ndani ya ukumbi kwamba baadhi ya washiriki walikuwa wamevaa skafu zilizoandikwa maneno “Palestina Huru”.
Mkutano huu unafanyika kwa ushiriki wa wawakilishi wa wafanyakazi, waajiri na serikali kutoka nchi 187 wanachama wa ILO, na unajadili masuala yanayohusiana na mustakabali wa dunia ya kazi.
Maoni yako