Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Mkuu wa Jaafari na mwanazuoni mashuhuri wa Lebanon, katika ujumbe wake kwa Rais wa Lebanon, Jenerali Joseph Aoun, amesema: Yeyote anayehimiza Muqawama kujiondoa kusini mwa mto huku wakati huohuo asidai kuondoka kwa jeshi la Kizayuni, huyo si mwakilishi wa Lebanon wala wa nyanja zake za mamlaka ya kitaifa.
Katika ujumbe huo imeelezwa: Wewe uko katika nafasi ambayo inapaswa kuwaleta watu pamoja, si kuwagawa; la sivyo utapoteza uhalali wako wa kitaifa. Hatutaki upoteze nafasi yako kama mhimili wa maslahi ya Lebanon, kutokana na mtazamo huu, tunakushauri kuachana na misimamo kama hii ambayo haistahili hadhi ya urais, kwa sababu taasisi ya urais imeundwa ili kuwa nembo ya mambo ya pamoja ya familia ya Lebanon, wala si sababu ya kuipasua vipande vipande.
Ameongeza kuwa: Kutetea makubaliano ya kiusalama na utawala wa Kizayuni hakufai kwa misimamo kama hii ambayo haiendani na hadhi ya urais, “Rais Nabih Berri” katika suala hili ni mfano na alama ya kihistoria, na wengi wanaweza kujifunza kutoka kwake, ee Mheshimiwa Rais, hebu tujiweke mbali na wazo la “uwakilishi”, kwa sababu mazungumzo kuhusu uwakilishi wa kitaifa na wa wananchi huanza kwa Rais Nabih Berri na Sheikh Naim Qassem, na jua halihitaji mwongozo; na simulizi la wale wasio na mwakilishi linajulikana, na hatutaki kulizungumzia.
Sheikh Qabalan amliendelea kusema: Taasisi yoyote ya kitaifa ambayo haiwakilishi Kusini, Dhahiyah na Biqaa, haiiwakilishi Lebanon, na taasisi za kitaifa ambazo haziwakilishi wananchi, nyanja za mapambano, mamlaka na harakati zao za kitaifa, hazina haki ya uwakilishi wa wananchi na wa kitaifa. Yeyote anayekabiliana na “Israel” gaidi katika vita vigumu, hapaswi kutoa mipango ya kiusalama kwa manufaa yake kwa gharama ya mamlaka ya Lebanon, wala hapaswi kujifunga kuubomoa mfumo wa Muqawama; Muqawama ambao uliikomboa nchi hii, serikali yake na maeneo yake mbalimbali ikiwemo “Ikulu ya Baabda”.
Mwanazuoni huyo wa Kishia wa Lebanon amesisitiza kuwa: Kama kusingekuwa na Muqawama wa kihistoria ambao katika vita hivi unalilisambaratisha ghala la silaha la Israel katika mipaka yote ya kusini, adui Muisraeli angefika hadi Ikulu ya Baabda, kwa hiyo, ee Mheshimiwa Rais, yeyote anayewakilisha wananchi wake hakubali kuwahamisha wakazi kutoka kusini mwa Lebanon. Yeyote anayozuia ulinzi wa kitaifa wa jeshi la Lebanon, halafu wakati huohuo atake Muqawama ujiondoe kusini mwa mto bila kudai kuondoka kwa wakati mmoja kwa jeshi la Kizayuni, huyo si mwakilishi wa Lebanon wala wa nyanja zake za mamlaka ya kitaifa.
Kwa upande mwengine Sheikh Qabalan, akijibu tuhuma na michezo ya kipropaganda isiyo na msingi, amesema: Iran haitumii marafiki wake dhidi ya maslahi ya nchi zao kama Washington inavyofanya, kinachotarajiwa kutoka kwako Mheshimiwa ni kulinda amani ya kiraia na mkataba wa kitaifa, si kuchochea moto wake.
Napenda kukumbusha kwamba; ni Iran ambayo iliitishia Israel gaidi kwamba ikiwa ingeishambulia Beirut, basi Iran ingeingia vitani, na aliyetoa mwanga wa kijani kwa Israel kuishambulia Beirut alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, si Iran, Iran hiyo hiyo ndiyo nchi ambayo mwaka 2000 ilitoa msaada mkubwa zaidi wa kihistoria kwa ukombozi wa kitaifa, na bado imesimama kwenye ahadi yake ili mipango ya Marekani na vita vikubwa vya Israel visiimeze Lebanon.
Maoni yako