Jumamosi 6 Juni 2026 - 12:43
Ayatullah al-Udhma Nouri Hamadani atoa salamu za rambirambi kuielekea Hawza ya Najaf

Hawza/ Ayatullah al-Udhma Nouri Hamedani ametuma salamu za rambirambi kufuatia kufariki kwa Ayatullah al-Udhma Fayyadh (ra), mmoja wa Maraji' wakubwa wa taqlid wa Najaf.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Matini ya ujumbe wa rambirambi wa Ayatullah Nouri Hamedani kufuatia kufariki kwa Ayatullah Fayyadh (ra) ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Kufariki kwa faqihi mtukufu, Ayatullah Fayyadh (ra), kumesababisha masikitiko na huzuni kubwa.

Bila shaka, kuondoka kwa shakhsia hii mashuhuri ya Hawza, ambae ametumia maisha yake yenye baraka katika njia ya kueneza utamaduni wa Ahlul-Bayt (as), na ambaye ameitumikia dunia ya Kiislamu kupitia kulea wanafunzi na kuandika kazi zenye thamani kubwa, kunahesabiwa kuwa ni hasara kubwa sana.

Mimi ninatoa pole kwa kufariki kwa Marjaa huyu mtukufu kwa Mashia wote na Hawza zote za kielimu, hususan Hawza kubwa ya Najaf pamoja na familia yake tukufu, na ninamuomba Mwenyezi Mungu amuinulie daraja marehemu huyu mwema.

15 Khordad 1405 H.S./ June 6 2026

Hussein Nouri Hamadani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha