Jumatatu 18 Mei 2026 - 23:00
Kupata shahada Izzuddin Al-Haddad kumeweka wazi uvunjaji wa ahadi na usaliti wa wavamizi

Hawza/ Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa kupata shahada Izzuddin Al-Haddad, kamanda wa Brigedi ya Izzuddin Al-Qassam, alisisitiza: Kupata shahada mujaahid huyu shupavu ni muhuri mwingine wa kuthibitisha uvunjaji wa ahadi wa wahalifu hawa Wakizayuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe alioutoa huku akisisitiza kuwa, irada ya chuma ya watu wa Ghaza haiwezi kuvunjwa na itashinda dhidi ya kambi ya dhulma na uhalifu, amesema: Kupata shahada “Izzuddin Al-Haddad”, kamanda jasiri wa Brigedi za Izzuddin Al-Qassam, pamoja na mkewe na binti yake, katika wakati ambao usitishaji vita wa Ghaza ulikuwa na sura ya udanganyifu kupitia ahadi za uongo za adui, kwa mara nyingine tena kumeweka wazi uvunjaji wa ahadi na usaliti wa wavamizi.

Ujumbe wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kufuatia kupata shahada Izzuddin Al-Haddad, kamanda wa Brigedi za Izzuddin Al-Qassam, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Katika moyo wa giza la vita na katikati ya kelele za miaka mitatu ya muqawama wa Palestina baada ya operesheni ya kihistoria ya “Tufani ya Al-Aqsa”, Ghaza shujaa, kama johari inayong’aa, imeipa maana subira na uthabiti, na imeyachochea mataifa mbalimbali katika pembe zote za dunia, hata huko Ulaya na Marekani, kuungana nayo. Wanaume na wanawake wenye ghera wa Palestina, kwa kutegemea imani na uimara wa miaka mitatu, wamesimama kama mlima imara mbele ya uhalifu wa kinyama kabisa wa zama za kati wa adui Mzayuni, wapiganaji mashujaa wa Hamas, kwa kuongozwa na aya tukufu: “رجال صدقوا ما عاهدوا الله علیه فمنهم من قضی نحبه ومنهنم من ینتظر و ما بدلوا تبدیلا” hawakuvunja ahadi yao kwa Mwenyezi Mungu, na katika njia hii ni wangapi wametoa maisha yao matamu muhanga, na ni wangapi wamebakia wakisubiri ushindi wa mwisho huku wakidumu katika ahadi yao.

Kwa mara nyingine tena, mkono wa kihalifu wa utawala katili wa Kizayuni umechafuliwa kwa damu safi ya mmoja wa mujāhidina wakubwa na mashujaa wa muqawama, “Izzuddin Al-Haddad”, kamanda jasiri wa Brigedi za Izzuddin Al-Qassam. Kupata shahada kwake, pamoja na mkewe na binti yake, katika wakati ambao usitishaji vita wa Ghaza ulikuwa na sura ya udanganyifu kupitia ahadi za uongo za adui, kwa mara nyingine tena kumeweka wazi uvunjaji wa ahadi na usaliti wa wavamizi.

Mujaahid huyu shupavu, ambaye ametumia maisha yake katika kupambana na wavamizi, iwe katika medani ya vita au katika magereza ya madhalimu wa Kizayuni, na ambaye pia amewatoa vijana wake wawili mashujaa katika njia hii, ni nembo ya uthabiti na kusimama kidete kwa watu wa Palestina.

Ingawa historia ya wavamizi wa Baytul-Maqdis na Qibla ya kwanza ya Waislamu imejaa uhalifu na khiyana, lakini kupata shahada kamanda huyu mkubwa katika kipindi cha usitishaji vita ni muhuri mwingine wa kuthibitisha uvunjaji wa ahadi wa uhalifu wa Wazayuni hao.

Bila shaka, ahadi ya Mwenyezi Mungu haivunjiki, na kwa kuendelea kwa njia ya muqawama, hatima ya taifa na ardhi ya Palestina itaamuliwa na watoto wake wenye ghera. Ushindi huu utaambatana na kuangamizwa kwa wavamizi wa Palestina, kuondolewa kwa uvimbe wa saratani wa utawala wa Kizayuni, kuinuliwa kwa Wapalestina mashujaa na wenye muqawama, pamoja na kuachiwa huru kwa Quds Tukufu, na adui huyu mdanganyifu na mwenye tabia ya mbwa mwitu wa Kizayuni lazima awe ameuelewa vizuri ukweli huu kwamba irada ya chuma ya watu wa Ghaza haiwezi kuvunjwa na itashinda dhidi ya kambi ya dhulma na uhalifu.

Katika njia hii yenye milima na mabonde, tunakumbuka na kuuenzi muqawama, uthabiti na kusimama kidete kwa watu wa Ghaza, makamanda na wapiganaji wa Hamas, pamoja na mashahidi watukufu wa Palestina.

Na kwa mara nyingine tena tunasisitiza juu ya uungaji mkono na ushirikiano usio na mipaka wa taifa kubwa la Iran, hasa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa muqawama huu wenye fahari, wenye nguvu na wa kihistoria, na katika njia hii tukufu hatutasita kufanya juhudi zozote

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha