Jumamosi 16 Mei 2026 - 15:00
Hatutaondoka barabarani mpaka adui ashindwe kikamilifu

Hawza/ Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Qum, huku akirejelea umuhimu wa uwepo wa wananchi mitaani, alisema: Leo kwa amri ya Walii Faqihi hatutaondoka mitaani mpaka tutakapowapigisha magoti maadui kwa ajili ya kuulinda Uislamu na Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saeedi katika khutba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 25 Ordibehesht 1405 (15 May 2026) iliyofanyika katika Msalla wa Quds mjini Qum, akifasiri kauli isemayo: “Uwanja wa mapambano ni wenu, barabara ni yetu”, alisema: Usiku mmoja tu hatukutoka nje, maadui walichoma misikiti, Qur’ani na Husseiniyya; kwa mtindo wa Daesh wakawakata vichwa na kuwachoma moto wananchi wasio na hatia; walivamia vituo vya Basij, vituo vya vikosi vya usalama, benki, magari ya wagonjwa, mali za wananchi na kadhalika, na wakavichoma moto.

Aliendelea kusema: Usiku mmoja tu hatukutoka nje, wakaanzisha fitna iliyokuwa utangulizi wa mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni, na wakawaua kishahidi mamia ya watoto na wasichana wasio na hatia, na zaidi ya watu 5000 wa Iran waliodhulumiwa waliuawa kishahidi katika machafuko ya ndani na Vita vya Ramadhani. Lakini leo kwa amri ya Walii Faqihi, hatutaondoka mitaani mpaka tutakapowapigisha magoti maadui kwa ajili ya kuulinda Uislamu na Iran.

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: Sisi tuko chini ya amri ya Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Wanajeshi, Ayatullah al-Udhma Sayyid Mujtaba Khamenei, na katika nyanja zote ikiwemo diplomasia tunapambana na maadui, na tutawapa pigo kubwa.

Mwakilishi wa Walii Faqihi mjini Qum alisisitiza: Kwa mujibu wa alivyosema Shahidi Suleimani, sisi ni taifa la Imam Hussein (a.s), na kauli ya taifa la Imam Hussein (a.s) ni: "Udhalili uwe mbali nasi".

Alisema: Utawala wa Iran juu ya Mlango wa Hormuz unaashiria ukweli utakaojitokeza katika siku zijazo zisizo mbali, tunatumaini mwisho wa ubabe wa Marekani utaandikwa kwa mikono ya Iran katika Mlango wa Hormuz, na kama Firauni alivyozama katika Mto Nile, Firauni wa zama zetu yaani Trump mwenye mawazo ya udanganyifu na mhalifu, aangamie katika maji ya Ghuba ya Uajemi.

Msimamizi wa Haram Tukufu ya Bibi Ma’suma (a.s), huku akirejelea shahada ya Imam Jawad (a.s), alisema: Mwenendo wa Imam Jawad (a.s) kwa wananchi wavumilivu na wenye kusimama imara wa Iran, ambao wako katika njia ya kuhifadhi heshima na uhuru wao huku wakikabiliwa na tufani kali za matatizo, una mambo mawili muhimu.

Jambo la kwanza: Azma katika kilele cha ujana

Alisema: Imam Jawad (a.s) alithibitisha kwamba; ukubwa hauko katika umri bali uko katika kusimama imara juu ya malengo na misingi. Huu ni ujumbe wa matumaini kwa kizazi cha vijana kwamba; katika kilele cha matatizo, vikwazo na mashinikizo wanaweza kuvunja njia zilizofungwa.

Jambo la pili: Ukarimu na usawa katika matatizo

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliendelea: Lakabu ya “Jawad” alipewa kwa sababu katika mazingira magumu zaidi ya kisiasa na mzingiro wa kiuchumi alikuwa ni kimbilio la waliodhulumiwa. Mafunzo ya leo ya Imam Jawad (a.s) kwetu ni mshikamano wa Kiimani, kwamba katika hali hizi ngumu tusiachiane mikono.

Akirejelea kumbukumbu ya ndoa ya Imam Ali (a.s) na Bibi Fatima (a.s), alisema: Maisha ya Imam Ali (a.s) na Bibi Fatima (a.s) ni mfano mzuri kabisa wa familia katika mizani ya Kiislamu. Ndoa hii ya mbinguni ina mafundisho katika nyanja tatu kuhusu changamoto kuu za jamii yetu ya leo.

Nyanja ya kwanza: Muungano, kheri nyingi na baraka

Alisema: Ndoa ya nuru hizi mbili za Mwenyezi Mungu ni mfano wa kuungana kwa bahari mbili, ambazo matokeo yake yalikuwa ni kuendelea kwa kizazi kitakatifu cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuvuma kwa upepo wa Uimamu duniani, somo kubwa la ndoa hii ni urahisi wa maisha, leo ambapo vikwazo vya kiuchumi na anasa vimekuwa kizuizi kwa ndoa na uzazi, kurejea kwenye mfano wa Alawi na Fatimi maana yake ni kwamba; utajiri wa kweli wa familia hauko katika anasa bali uko katika usafi wa moyo, imani na kuwa na watoto wema.

Nyanja ya pili: Kuzaa watoto

Aliongeza: Katika mantiki ya Uislamu, mtoto si tu kuja mtu mpya katika jamii, bali ni juhudi za kuhifadhi na kuiendeleza jamii ya Kiislamu. Leo suala la kupungua  idadi ya watu limekuwa mgogoro wa uwezo wa taifa letu, jamii inayokuwa ya wazee hupoteza ubunifu, uchangamfu, uwezo wa kujilinda na nguvu za ujenzi, leo kuzaa watoto ni jihadi ya kivitendo na ya kubainisha ukweli.

Nyanja ya tatu: Kukabiliana na utamaduni wa upweke na ubachela

Alisema: Dunia ya leo inatangaza ubachela na kutokuwa na watoto kama uhuru, hali ya kuwa mfano wa Fatima unatufundisha kwamba ukamilifu wa mwanadamu uko katika kukubali jukumu la maisha, idadi ya vijana ndiyo msukumo wa uchumi na ngome madhubuti dhidi ya tamaa za maadui, tunahitaji kizazi ambacho kwa malezi ya Alawi kirithi ushujaa kutoka kwa Imam Ali (a.s) na uthabiti kutoka kwa Bibi Zahra (a.s) ili kifikishe mzigo mzito wa kujenga ustaarabu kwenye lengo lake.

Mwakilishi wa Walii Faqihi mjini Qum, huku akiadhimisha kumbukumbu ya Mashahidi wa Huduma na shahada ya Ayatullah Raisi pamoja na wenzake, aliongeza kuwa: Tukio hili chungu lilifungua ukurasa mpya wa utamaduni wa huduma katika historia ya Mapinduzi.

Mafunzo kutoka kwa Mashahidi wa Huduma /Tafsiri mpya ya usimamizi wa kijihadi

Alisema: Shahidi Raisii alionesha kwamba; dawati la huduma la kiongozi mkuu wa mfumo haliko ndani ya vyumba vilivyofungwa, bali liko kwa wananchi, kwa sababu hiyo aliitwa Sayyid ash-Shuhadaa wa huduma, kwani hakupata utulivu katika njia ya kutatua matatizo ya wananchi, somo lake kubwa kwa viongozi ni kuwa pamoja na wananchi na kujiepusha na maisha ya kifahari.

Diplomasia ya heshima na nguvu

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: Shahidi Amir-Abdollahian alikuwa mfano wa diplomasia ya muqawama, alithibitisha kwamba; medani ya mapambano na diplomasia ni vipengele viwili vikuu visivyotenganishwa.

Mfano wa Imamu wa Ijumaa wa kiwango bora

Aliendelea kisema: Shahidi Ayatullah Al Hashem huko Tabriz alifafanua upya maana ya baba wa kiroho wa mji, na akaifanya Swala ya Ijumaa kuwa kimbilio la uhakika kwa ajili ya jihadi ya kubainisha ukweli na kuwahudumia wananchi.

Shahada kwa ajili ya wananchi wenye kusimama imara

Alisisitiza kiwa: Kupaa kwa damu ya mashahidi hawa kulikuwa na ujumbe kwa wananchi kwamba; malipo ya nia ya kweli ni shahada, na jamii ilikopa umoja na uthabiti kutoka katika msiba huu, damu ya mashahidi hawa haikusababisha dosari yoyote katika uendeshaji wa nchi, bali iliimarisha zaidi azma ya taifa ya kuendelea katika njia ya maendeleo.

Khatibu wa Ijumaa wa Qum, huku akiadhimisha Siku ya Mwezi mweekundu, alisema: Mwezi mwekundu ni dhihirisho la kujitolea kusikokuwa na mipaka na ni tegemeo salama ambalo katika nyakati ngumu zaidi hurudisha matumaini na tabasamu katika nyoyo na macho ya waliopatwa na maafa.

Pia huku akiadhimisha Wiki ya Afya alisema: Tunawashukuru wafanyakazi wote na wahudumu wa sekta ya afya, Ninyi mpo Qum, katika Haram ya Ahlul Bayt (a.s), kitovu cha wapenzi wa kizazi cha Mtume Muhammad na mji wa Maraji' wakubwa pamoja na chimbuko la Mapinduzi; kwa sababu hiyo kiwango cha afya kinachotarajiwa kutoka mkoa wa Qum ni cha juu zaidi kuliko mikoa mingine.

Muungurumo wa taifa ulikuwa mfano wa nusura ya Mwenyezi Mungu

Ayatullah Saeedi katika khutba ya kwanza, huku akirejelea aya isemayo: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu”, alisema: Uchaji Mungu, tofauti na baadhi ya majukumu ya kidini, hauhusiani na wakati maalumu au mtu maalumu; bali wote waliowajibishwa wanapaswa katika hatua zote za maisha kuwa wachamungu katika njia bora kabisa.

Alisema: Mwenyezi Mungu katika aya ya 21 ya Suratul-Fath anasema:

“Na mengine hamwezi kuyapata bado, Mwenyezi Mungu amekwisha yazingia. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.”

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: Katika siku hizi tuko katika maombolezo ya Imamu shahidi wa Mapinduzi, lakini msiba mkubwa zaidi ni kwamba hakuna aliyefahamu vipimo vya uwepo wake, katika vipindi mbalimbali vinavyoandaliwa, baadhi ya watu huonesha sehemu ndogo ya sura ya mtu huyo mkubwa, pia katika siku hizi tumeshuhudia huzuni ya shahada ya wapiganaji, wanasayansi na watoto waliodhulumiwa wa shule ya Minab, usaliti mkubwa uliofanywa na nchi za Ghuba, hususan Imarati, na kuifanya eneo la pili la Israel, ulikuwa pia huzuni nyingine tuliyoishuhudia.

Alisema: Mwenyezi Mungu katika aya ya 21 ya Suratul-Fath anatufungulia mlango wa nuru na matumaini na anasema; kuna ushindi ambao kwa mtazamo wa kawaida hamna uwezo wa kuupata, kutafakari aya hii ndiyo ufunguo wa kuelewa mabadiliko ya leo.

Msimamizi wa Haram Tukufu ya Bibi Ma’suma (a.s) aliongeza kusema: Adui alikuja na zana zote za kijeshi na kimedia ili kuumaliza mfumo, walifikiri kwamba kwa shahada ya Kiongozi shahidi wa Mapinduzi, wataiangusha Iran, lakini walighafilika kuhusu hesabu ya nguvu kubwa ya Mwenyezi Mungu.

Alisema: Ni nguvu gani ya kibinadamu iliyoweza kudhani kwamba shahada ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu haitasababisha kuporomoka kwa Mapinduzi, bali itasababisha mafuriko ya uwepo wa wananchi mitaani yatakayotikisa misingi ya Ikulu ya Nyumba nyeupe?

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliendelea: Adui alijaribu kuwatoa wananchi katika njia ya muqawama, lakini taifa letu katikati ya uwanja lilitengeneza hamasa ambayo historia haijawahi kuona mfano wake, uwepo wa kishujaa wa wananchi mitaani ni kiapo kipya cha utiifu kwa malengo ya Imam marehemu na utiifu kwa khalifa wake mwema, Ayatullah al-Udhma Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, jambo lililoonesha kwamba; bendera hii si tu haitadondoka chini, bali kwa damu zinazomwagika katika njia ya Mwenyezi Mungu itaendelea kuinuliwa kwa nguvu zaidi kuliko hapo kabla, uwepo huu wa wananchi ni mfano wa nusura ya Mwenyezi Mungu inayotokea zaidi ya hesabu za kimada.

Mwakilishi wa Walii Faqihi mjini Qum alisisitiza: Marekani na Wazayuni wa kimataifa wajue kwamba ingawa tunamlilia Kiongozi wetu, lakini mikono yetu ipo juu ya vichocheo vya silaha na nyoyo zetu zimejaa matumaini kwa ahadi ya kweli ya Mwenyezi Mungu.

Aliongeza: Taifa letu ni mfano wa aya ya 21 ya Suratul-Fath, kwamba; Mwenyezi Mungu ametuhifadhia ushindi ambao adui hata haudhanii, Kusimama imara na uwepo wa mamilioni ya wananchi katika ngome na mitaa haukuwa jambo la kawaida, bali ilikuwa nusura ya Mwenyezi Mungu iliyotuliza nyoyo zilizovunjika na zenye hofu baada ya shahada ya kidhulma ya Kiongozi wa Mapinduzi, ili adui asiweze kutumia vibaya mshtuko wa mwanzo.

Khatibu wa Ijumaa wa Qum alisema: Kosa la mahesabu ya adui pia ni nusura nyingine kubwa ya Mwenyezi Mungu, maadui kwa kuivamia Iran hawakubomoa tu heshima yao ya bandia duniani na hata ndani ya Marekani, bali walijichimbia kaburi lao wenyewe katika eneo hili, na wakasababisha kuundwa kwa umoja ambao haujawahi kushuhudiwa katika eneo hili na duniani dhidi ya Trump mcheza kamari na “nguruwe mchafu”.

Akirejelea aya ya 21 ya Suratul-Fath aliongeza: Kuwafukuza Mayahudi wa majumba na matajiri wa Khaybar halikuwa jambo lililotarajiwa kwa Waislamu wa Madina, lakini Mwenyezi Mungu kwa mara ya kwanza alifanya watu maskini wa Madina wawashinde wenye majumba wa Kiyahudi wa Khaybar na kuwafukuza.

Mwakilishi wa Walii Faqihi mjini Qum alikumbusha: Leo pia kundi hili lenye ukaidi, ukafiri, uvamizi, uporaji na uuaji wa watoto litang’olewa kutoka katika eneo hili kwa mikono ya watu ambao Mwenyezi Mungu amesema kuwahusu:

“Anawapenda nao wanampenda; wanyenyekevu kwa Waumini na wakali dhidi ya makafiri.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha