Alhamisi 14 Mei 2026 - 16:15
Maandamano ya wananchi wa Stockholm dhidi ya jinai za Israel huko Ghaza na Lebanon

Hawza/ Mamia ya waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu wa Sweden ili kupinga operesheni za kijeshi za utawala wa Israel za kuwaua watu wa Ghaza na Lebanon, na wakataka kusitishwa kwa mauaji ya raia pamoja na kuchukuliwa hatua pana zaidi za kimataifa dhidi ya utawala huo wa umwagaji damu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mkusanyiko huo ulifanyika katika bustani ya Observatorielunden, ambapo washiriki walikuwa wamebeba bendera za Palestine, Lebanon na Iran, pamoja na mabango yaliyokuwa na kaulimbiu kama: “Sitisheni kuwaua raia”, “Malizeni mzingiro wa chakula dhidi ya Ghaza” na “Sitisheni mashambulizi dhidi ya Lebanon na Iran”.

Maandamano hayo, ambayo yaliandaliwa na muungano wa makundi ya kiraia na ya wananchi, yalionesha ukosoaji wa wazi dhidi ya mwitikio hafifu wa kimataifa kuhusu hali mbaya na inayozidi kuwa hatari ya kibinadamu duniani kutokana na jinai za utawala wa Kizayuni unao mwaga damu.

Miongoni mwa waliozungumza alikuwa mwanaharakati wa kisiasa wa Swiden, Dror Feiler, ambaye alilaani sera za utawala wa Israel huko Ghaza na Lebanon, na pia aliishutumu kwa nguvu Jumuiya ya kimataifa kwa kile alichokiita ukimya wa makusudi.

Pia alikosoa mashambulizi ya pamoja ya Israel na Marekani dhidi ya Iran, na kuyataja kuwa ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, huku akiiomba serikali ya Sweden kusitisha haraka iwezekanavyo uuzaji wa silaha kwa Israel.

Waandamanaji pia walipinga msimamo usio wa kibinadamu wa Greece kuhusu hatua za Israel dhidi ya meli ya kimataifa ya Samud, na wakaeleza kutoridhishwa kwao na unafiki pamoja na mienendo isiyo ya kiungwana ya viongozi wa serikali dhidi ya wananchi wanaoiunga mkono Palestine.

Chanzo: EUPAC

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha