Jumatatu 11 Mei 2026 - 13:51
Kongamano la 31 la Kimataifa la Qur’ani Tukufu lafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania

Hawza/ Chuo Kikuu cha Jaamiatul Mustafa kilichopo nchini Tanzania kiliadhimisha Kongamano la 31 la Kimataifa la Qur’ani Tukufu, likiwa ni tukio kubwa, adhimu na la kihistoria lililolenga kukuza elimu, maadili mema na mshikamano wa Kiislamu kupitia Kitabu Kitakatifu cha Qur’ani, nuru ya maisha ya mwanadamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kongamano hilo la kimataifa lilifanyika jana, Jumapili, tarehe 10 Mei 2026, jijini Dar es Salaa, likiwa limekusanya waumini wengi, wasomi, wanazuoni na shakhsia mbalimbali mashuhuri za kielimu kutoka maeneo tofauti ya ndani na nje ya nchi.

Tukio hilo adhimu na lenye baraka tele lilitajwa kuwa miongoni mwa majukwaa muhimu na yenye ushawishi mkubwa katika kukuza uelewa sahihi wa mafundisho ya Qur’ani Tukufu, sambamba na kuimarisha umoja, upendo na undugu miongoni mwa Waislamu.

Kupitia kongamano hilo, washiriki walipata fursa ya kujifunza kwa kina, kubadilishana uzoefu wa kielimu, pamoja na kushuhudia vipaji vya hali ya juu na vya kuvutia katika sekta ya usomaji wa Qur’ani.

Miongoni mwa wageni mashuhuri walioshiriki kongamano hilo na kulipamba jukwaa kwa sauti tamu na visomo vya kugusa nyoyo, ni wasomaji wazawa kutoka Tanzania, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan.

Vilevile, mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano na Amani (JMT), Sheikh Alhad Mussa. Aidha, hakukosekana Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania (TIC), Maulana Hemedi Jalala Mwakindenge, ambaye mbali na visomo vizuri vya Qur’ani, uwepo wake uliongeza hamasa, heshima na manufaa makubwa kwa washiriki na waliohudhuria.

Wasimamizi wa kongamano hilo walisema kuwa; maandalizi yalifanyika kwa umakini mkubwa na kiwango cha hali ya juu, yakilenga kuhakikisha kuwa tukio hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa, ustadi wa kipekee na mvuto wa aina yake, huku likiacha alama isiyofutika katika nyoyo za washiriki wote. Vile vile pia, waliwashukuru waumini na wananchi kwa ujumla kwa kujitokeza kwa wingi, kushiriki katika tukio hilo adhimu la kiroho, kielimu na kijamii.

Kwa hakika, Kongamano la 31 la Kimataifa la Qur’ani Tukufu lilikuwa chemchemi ya nuru, maarifa, utulivu wa moyo na mshikamano, huku likiimarisha zaidi nafasi ya Tanzania katika ramani ya kimataifa ya kukuza, kusambaza na kuhifadhi mafundisho ya Qur’ani Tukufu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Kongamano la 31 la Kimataifa la Qur’ani Tukufu lafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania

Kongamano la 31 la Kimataifa la Qur’ani Tukufu lafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania

Kongamano la 31 la Kimataifa la Qur’ani Tukufu lafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania

Kongamano la 31 la Kimataifa la Qur’ani Tukufu lafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania

Kongamano la 31 la Kimataifa la Qur’ani Tukufu lafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania

Kongamano la 31 la Kimataifa la Qur’ani Tukufu lafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha