Jumamosi 4 Aprili 2026 - 17:40
Watu wote washiriki katika harakati ya pamoja ya kuwepo uwanjani/ Kusimamishwa masomo hadi taarifa nyingine

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli amesisitiza kuwa: Inafaa watu wote washiriki katika harakati ya pamoja ya kuwepo uwanjani, na kila mtu, hasa wanazuoni wakubwa wa dini, wawe na mchango mkubwa zaidi katika kutekeleza majukumu yao ya Kimungu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina Lake Aliyetukuka

Kwa heshima kubwa kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya juu waliopo katika tafiti za Hawza,

Baada ya salamu na maamkizi, pamoja na kutakieni ushindi na ufanisi mashujaa na wenye nyoyo jasiri wa kambi ya haki dhidi ya batili;

Sasa ambapo kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, ishara za kudhihirika kwa irada ya Mwenyezi Mungu katika ushindi na nusra ya jeshi la Mwenyezi Mungu, na kudhalilika na kushindwa kwa nguvu za kiburi cha dunia na Uzayuni wa kimataifa zimeonekana wazi;

Inafaa watu wote kushiriki katika harakati hii ya pamoja ya uwepo, na kila mtu, hasa wanazuoni wakubwa wa dini, wawe na mchango mkubwa zaidi katika kutekeleza majukumu yao ya Kimungu.

Kwa msingi huo, tafiti za kielimu zimeathiriwa na harakati hii ya Kimungu, na hadi taarifa nyingine itakapo tolewa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu azidishe mafanikio na ushindi kwa Ummah na mfumo wa Kiislamu.

Abdullah Jawadi Amoli

14 Farvardin 1405

Zingatia: Inaarifiwa kwamba masomo ya Mtukufu Ustadh yamesimamishwa hadi taarifa nyingine itakapo tolewa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha