Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Zakzaky katika mkutano na kundi la wanaharakati wa kitamaduni na kisiasa wa Nigeria, alilaani mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na akatoa wito kwa ulimwengu wa Kiislamu kuiunga mkono Iran.
Mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya Iran
Katika kueleza mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, alisema: “Tangu mwezi wa Rajab, maadui walikuwa wamekusanya silaha katika maeneo yanayozunguka Iran na kuandaa mazingira ya mashambulizi. Mashambulizi ya kwanza yalifanywa dhidi ya nyumba ya Sayyid Qaed na shule za wasichana na wavulana, ambapo makumi ya wanafunzi na makumi ya raia wasio na hatia walipata shahada.”
Aliongeza, akieleza kwamba baadhi ya mashambulizi hayo yalifanywa kutoka ardhi ya Imarati, Bahrain na baadhi ya nchi za Kiislamu:
“Mashambulizi dhidi ya nyumba ya uongozi yalifanywa kutoka Imarati, na mashambulizi dhidi ya wanafunzi yalitoka Bahrain. Hali hii ni wakati ambapo kulikuwa na makubaliano kati ya nchi hizi na Iran kwamba ardhi zao haitatumika kwenye mashambulizi dhidi ya Iran.”
Kulenga uchumi wa Iran
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alisema kuwa maadui baadaye walilenga miundombinu ya uchumi wa Iran, akisema:
“Kuanzia viwanda vya chuma na saruji hadi vituo vya kuzalisha umeme, vililengwa ili kudhoofisha uchumi wa Iran. Iran nayo ilitoa majibu ya kulipiza dhidi ya vituo vinavyohusiana na adui katika nchi za Kiarabu.”
Alisisitiza kuwa: “Iran haijawahi kulenga raia wa kawaida, na majibu yake yalikuwa tu dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani; kwa sababu Marekani ilitumia ardhi ya nchi hizi kwa ajili ya mashambulizi.”
Sababu kuu ya vita
Kwa mujibu wa Sheikh Zakzaky, Wazayuni kwa zaidi ya miaka 40 walikuwa wamkisubiri rais wa Marekani ambaye angeingia vitani dhidi ya Iran:
“Trump, kwa kuchochewa na Israel, alichukua hatua hiyo. Walidhani kwamba shambulio la Marekani lingeiangamiza Iran; hivyo sababu kuu ya uadui huu ni nafasi ya Iran katika kuzuia kuundwa kwa Israeli Kubwa.”
Kambi za Marekani katika nchi za Kiarabu
Aligusia uwepo wa kijeshi wa Marekani katika Ghuba ya Uajemi na kusema:
“Kambi za Marekani hazikuundwa kwa ajili ya kulinda nchi za Kiarabu; bali ni sehemu ya mpango wa kulinda mradi wa Israeli Kubwa.”
Nafasi ya Iran katika kuisaidia Palestina
Sheikh Zakzaky alisisitiza kwamba; Iran, kwa msingi wa hisia ya wajibu wa Kiislamu, inaiunga mkono Palestina, akisema:
“Iran haijawahi kuwa na mtazamo wa kimadhehebu, bali imewasaidia Wapalestina kama Waislamu wanaodhulumiwa.”
Alikumbusha kuwa; msaada huu ulisababisha kuundwa kwa makundi ya muqawama katika Iraq, Lebanon, Yemen na maeneo mengine.
Wito wa kuuombea ushindi wa mhimili wa muqawama
Mwisho, Sheikh Zakzaky aliwataka Waislamu kuuombea ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na makundi ya muqawama, na akasisitiza kusoma Surah Yasin, Al-Fatiha na dua za Sahifa Sajjadiyya.
Maoni yako