Jumatano 1 Aprili 2026 - 07:00
B'aqir Darw'ish: Mamlaka za Bahrain hazina idhini ya wananchi

Hawza/ Mkuu wa "Chama cha Bahrain cha Haki za Binadamu" amekosoa sera za serikali ya Bahrain katika kudhibiti maoni ya umma.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, B'aqir Darwish, Mkuu wa "Chama cha Bahrain cha Haki za Binadamu", amekosoa sera za serikali ya Bahrain katika kudhibiti maoni ya umma na kuishutumu kwa kutafuta fursa za kutoa taarifa zenye shutuma, kuharibu sifa, na kutoa wito wa kuongeza adhabu dhidi ya mazingira ya mapinduzi.

Darw'ish ameeleza kwenye akaunti yake kwenye mitandao ya kijamii kwamba; taarifa za uungaji mkono zinazochapishwa kupitia televisheni ya Bahrain na vyombo vya habari vya serikali si chochote isipokuwa kurudia kwa sauti ya Baraza Kuu la Ulinzi, ambalo ndilo linaloamua pekee, na hii haiakisi msimamo halisi wa wananchi.

Akiashiria kwamba sera za kiusalama zinazotegemea "ngumi ya chuma" badala ya kurekebisha makosa hazileti utulivu, amesisitiza kuwa; ushiriki wa kisiasa wa raia ndiyo njia halisi ya kufikia utulivu, na si kutegemea kambi za kijeshi ambazo lengo lao ni kulinda maslahi ya Marekani na Israel.

Darw'ish pia ameuliza kuhusu kiwango cha ushiriki wa raia katika kuamua sera za ndani na nje, na kusema kwamba; nchi inayotumia jela kumshughulikia yeyote anayechapisha tweet au kuchapisha tena maudhui fulani, haiwezi kudai kuwa ina idhini ya wananchi.

Mkuu wa Chama cha Haki za Binadamu amesisitiza kwamba; vyombo vya habari vya kimataifa vinatambua kuwa ushiriki wa Bahrain katika vita dhidi ya Iran hauoneshi msimamo mpana wa wananchi, na kwamba baadhi ya ripoti rasmi zinatayarishwa kwa mujibu wa maelekezo ya "Chumba cha Habari cha Usalama" katika Wizara ya Mambo ya Ndani; hata hadi Waziri wa Mambo ya Ndani mwenyewe haamini kila kinachorushwa kwenye televisheni ya Bahrain.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha