Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, Kiongozi Mtukufu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ametuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kuuawa kishahidi kwa Kamanda wa Jeshi la Majini, Alireza Tangsiri.
Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu
"Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi."
Kamanda shupavu na mwenye ujasiri wa Jeshi la Majini la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Generali Alireza Tangsiri, baada ya miaka mingi ya jitihada za kishujaa, ametunukiwa daraja la shahada.
Kuuawa kishahidi kwa kamanda huyo jasiri, askari wa Iran na mlinzi wa Uislamu katika mapambano ya Vita vya Tatu vya Kulazimishwa, ni kumbukumbu tukufu kwa watu mashujaa wa Bushehr, vijana wa eneo la Kusini, majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran, ambao daima wamekuwa walinzi wa uhuru na mipaka ya bahari ya Iran, hususan Ghuba ya Uajemi—hii ikiwa ni ithibati kubwa ya heshima ambayo, Mwenyezi Mungu akipenda, itawafanya waendelee kwa nguvu na uimara zaidi katika njia ya uwezo na uimara wa majini Iran.
Mimi ninatoa pongezi na rambirambi kwa kuuawa kishahidi kwa kamanda huyo shujaa kwa familia yake tukufu, wenzake wa karibu, na makamanda wa Jeshi la Majini na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe shahidi huyo daraja ya juu.
Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei
Maoni yako