Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Mohammad Saeedi katika khutba za swala ya Idi Tukufu ya Fitri iliyoswaliwa katika haram takatifu ya Bibi wa heshima, huku akibainisha kwamba; uangalizi wa neema za Mwenyezi Mungu juu yetu sisi watu huongezeka pale tunaposhikamana na uchamungu, alisema: Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani kwamba; "Lau watu wangeamini na kuwa na taqwa, tungelifungua milango ya baraka za mbinguni juu yao".
Aliongeza kwamba; mwezi mtukufu wa Ramadhani ni uzoefu mzuri wa kushikamana na taqwa, na akasema: Ujumbe wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kwamba, inawezekana katika siku zote za mwaka kujiepusha na yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu.
Imamu wa Ijumaa wa Qom, huku akirejelea dua ya Imam Sajjad (amani iwe juu yake) katika siku ya Idd al-Fitr, alisema: Alimwelekea Mwenyezi Mungu na kusema kwamba wale waliomwomba asiyekuwa Wewe wamepata hasara, na wale waliokaa katika milango ya asiyekuwa Wewe wameangamia, na wale waliotafuta neema kutoka kwa asiyekuwa Wewe wamepatwa na umaskini na njaa.
Alisema kwamba; taqwa ni silaha ambayo maadui hawana, na akaongeza: Watu wetu wanapambana kwa kutumia silaha hii, na tunapaswa kuthamini silaha hii ya kipekee na kuitumia.
Ayatollah Saeedi katika khutba ya pili, huku akibainisha kwamba; muumini anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho lazima atimize ahadi na kiapo chake, alisema: Ahadi na wajibu wetu wa kwanza ni kumtii Mwenyezi Mungu na kiongozi wa Mwenyezi Mungu, na mwaka huu ambapo kwa shahada ya kiongozi wetu mpendwa, uongozi wa mambo ya waumini na uimamu wa jamii umekabidhiwa kwa Ayatollah Imam Sayyid Mojtaba Husseini Khamenei, umma wa waumini wa Iran umeweka ahadi ya kusimama imara juu ya Wilayat al-Faqih na unasimama juu ya ahadi yake hadi mwisho wa uhai wake.
Maoni yako