Jumapili 15 Machi 2026 - 15:11
Abu Alaa Al-Wala’i: Kuondoka kwa Wamarekani 70,000 kutoka Mashariki ya Kati kulikuwa “kutoroka kwa vurugu”

Hawza/ Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhadaa ameelezea kuwa; kuondoka kwa makumi ya maelfu ya Wamarekani kutoka Mashariki ya Kati kuwa ni “kurudi nyuma kwa vurugu na kufanana na kukimbia”, na akaliona hilo kuwa, ni dalili ya kuongezeka kwa gharama za uwepo wa wavamizi katika eneo hilo pamoja na kuingia kwa Muqawama wa Kiislamu katika “hatua ya pili ya operesheni za ubora na za kuzuia”.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Abu Alaa Al-Wala’i, Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhadaa, katika ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa kijamii wa X, alielezea kuwa; kuondoka kwa takribani wanajeshi na raia wa Kimarekani wapatao 70,000 kutoka Mashariki ya Kati kuwa ni “kurudi nyuma kwa vurugu na kufanana na kukimbia”, na akasema kuwa; jambo hilo ni matokeo ya kuongezeka kwa gharama za uwepo wa wavamizi katika hatua ya pili ya operesheni za Muqawama ya Kiislamu.

Al-Wala’i alisisitiza kwamba; watu hao walijumuisha wanajeshi, wafanyakazi na raia wa Kimarekani ambao, kufuatia “majaribio yasiyofikiriwa vyema ya Marekani katika eneo hilo”, na katika mfumo wa kile kinachoitwa katika istilahi za kijeshi “kujipanga upya kuelekea uwanja wa ndege ulio karibu zaidi”, waliondoka Mashariki ya Kati.

Aliongeza kuwa; kuondoka huku kwa haraka kutaambatana na “kumbukumbu nzito” kwa Wamarekani; kumbukumbu ambazo kwa mujibu wake, kama ilivyokuwa kwa askari wavamizi baada ya shambulio la Marekani dhidi ya Iraq mwaka 2003, zitawaacha wengi wao wakikabiliana na athari za kisaikolojia kwa miaka mingi.

Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhadaa, akirejelea mabadiliko ya kiusalama katika eneo hilo, alisisitiza kuwa: ikiwa kuingia Asia ya Magharibi hapo zamani kulikuwa rahisi kwa Marekani, sasa—hasa katika hatua ya pili ya operesheni za Muqawama ya Kiislamu—kuondoka humo kumekuwa na gharama kubwa sana.

Abu Alaa Al-Wala’i pia alisema: hatua ya pili ya operesheni za Muqawama wa Kiislamu “ina malengo ya ubora na inaonesha kuhamishwa vita kuelekea katika kiwango kipya cha shinikizo na uzuiaji”.

Mwisho, alisisitiza kwamba; katika hali hii, “uwepo na kubaki kwa vikosi vya uvamizi katika eneo hilo kutazidi kuwa na gharama kubwa kwao kila siku”.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha