Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Vituo vya Kiutamaduni vya Imam Khomeini iliadhimisha kumbukumbu ya kupotea kwa Imam Musa Sadr pamoja na wenzake wawili katika makao yake makuu mjini Sur. Mkutano huu wa kielimu uliopewa anuani isemayo: “Vipengele vya Jamii Inayostahamili kutokana na mtazamo wa Imam Sadr” ulihudhuriwa na wabunge kutoka katika vikundi vya Uaminifu kwa Muqawama, Maendeleo na Uhuru, na pia wawakilishi wa Bunge akiwemo Hasan Izz al-Din na Ali Khreis, pamoja na nyuso mashuhuri, wanazuoni wa dini na kundi la wapenda masuala hayo.
Hasan Izz al-Din, mbunge na mjumbe wa Kikundi cha Muqawama, katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, alieleza baadhi ya vipengele vya mradi wa Imam Musa Sadr kwa mujibu wa mtazamo wake na utekelezaji wa kivitendo, akisisitiza kwamba tangu alipowasili nchini Lebanon, jambo la kwanza alilolifanya lilikuwa ni kurejesha heshima na hadhi stahiki ya madhehebu ya Kishia baada ya kutupwa pembezoni, kutawaliwa na kutegemezwa.
Akaongeza kusema: Imam Musa Sadr alianzisha Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia, taasisi za kielimu, na jumuiya kama vile al-Birr na al-Ihsan sambamba na mipango mingine. Baadaye alianza kuongeza uelewa kuhusu hatari ya adui wa Kizayuni na tamaa zake, akibainisha kwamba adui huyo ni adui muovu, chukizo na muhalifu, ambaye anasaidiwa na kuungwa mkono na waarabu pamoja na Magharibi.
Izz al-Din aliendelea kusema: Waarabu walikuwa na ushawishi mkubwa zaidi katika kukuza na kuimarisha utawala huo, na kama asemavyo msomi Jamal Hamdan, bila msaada huo, utawala huo usingeweza kudumu na kuendelea kuishi katika mazingira yenye uhasama kama haya.
Mwanachama huyo wa Kikundi cha muqawama alibainisha kuwa: Mtazamo wa Imam Sadr ulikuwa umejengwa juu ya misingi miwili mikuu, mbali na kuunda Kamati ya Kulinda Kusini, ambayo ilihusisha madhehebu na makundi mbalimbali ya Waislamu wa Kisunni, Wadruzi, Wakristo, Mashia, Waalawi, Waarmenia na makabila madogo bila kumtenga yeyote. Hili lilionyesha upeo wa fikra zake, elimu yake na imani yake katika uhalisia wa Lebanon, ambao aliishi nao kwa umakini na utaalamu mkubwa, aliunda kamati ya kulinda kusini.
Alisema pia: Imam Musa Sadr mara tu baada ya hapo alianzisha Harakati ya Waliodhulumiwa na baadaye Vikosi vya muqawama vya Lebanon (Amal), katika wakati ambapo mikanda ya umaskini na taabu ilikuwa imelikumba eneo la kusini mwa Beirut, mji mkuu na vitongoji vyake, na vilevile Lebanon yote kuanzia kusini hadi Bekaa ya Magharibi, kisha hadi Bekaa ya Kaskazini, Tripoli na Akkar.
Hasan Izz al-Din akabainisha kuwa: Harakati ya Waliodhulumiwa na muqawama ndizo zilikuwa msingi wa kuendeleza mradi wowote ule. Na alipoona Imam Sadr kwamba serikali imepuuza haki za kusini, imeshindwa kuwalinda watu na kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kitaifa, mwaka 1974 alitoa wito wa kufanya mkutano wa Baalbek, na huko alitoa kauli mbiu: “Silaha ni pambo la mwanaume.”
Akasema: Miezi michache baadaye, Imam Musa Sadr aliitisha mkutano katika uwanja wa Qasam mjini Sur ambapo alitangaza waziwazi: “Viongozi wanadanganya na ni walaghai, nami nitaendelea kushirikiana na watu wote waaminifu na wazalendo mpaka tupate kile kinachohitajika kwa ajili ya kusini.”
Mbunge wa Lebanon alibainisha kwamba Imam Sadr aliitaka serikali ya Lebanon kujenga makimbilio kwa ajili ya watu wa kusini na kuwapata waungaji mkono kwa jeshi la Lebanon ili kufidia upungufu, uzembe na kutochukua hatua ambayo kihistoria Lebanon imekuwa ikiipitia kutokana na kutawaliwa na moja ya vipengele vya kikabila vilivyokuwa vikiongoza wakati huo.
Maoni yako