Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Ali Fadhlallah, Imamu wa Ijumaa wa Beirut, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kutoweka kwa Imam Musa Sadr alisema: “Kutoweka kwa Imam Musa Sadr, kutokana na nafasi yake ya kuleta umoja wa kitaifa na Kiislamu, na kuunga mkono kwake malengo ya haki, hususan lengo la Palestina, ni hasara kubwa.”
Aidha aligusia uhusiano wa kindugu na wa karibu uliokuwa ukimunganisha Imam Musa Sadr na marehemu Ayatullah Sayyid Muhammad Hussein Fadhlallah, akakumbushia kuhusu mikutano ya Imam Musa Sadr na yeye katika mji wa Nabaa kwa ajili ya kushauriana na kujadili masuala mengi, pamoja na ushiriki wake katika hafla zilizokuwa zikifanyika huko.
Mwisho, Sayyid Ali Fadhlallah alisema: “Waliunganishwa na kipengele cha misingi ya pamoja, nacho ni mapokezi na uwazi wao wa mawazo ya kibinadamu na kufikisha ujumbe wa kukuza umoja, ukaribu na mazungumzo kati ya makundi mbalimbali ya kidini na kijamii.”
Maoni yako