Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, huu ulikuwa ndio mgomo wa kwanza wa pamoja wa vikundi vya habari ambapo zaidi ya waandishi wa habari na vyombo 250 vya habari, kwa uratibu wa kikundi kinachoitwa Waandishi Vijana (RSF) kutoka nchi 70 duniani, walichukua hatua ya kuweka kurasa zao weusi na kusitisha matangazo yao, ili kupinga mauaji ya waandishi wa habari yanayofanywa na Israel mhalifu.
Vituo vingi vya redio na televisheni vilishiriki katika harakati hii ya pamoja na kusitisha vipindi vyao kwa wakati mmoja na kuweka kurasa zao nyeusi, baadhi yao pia walionesha bendera ya mshikamano na Palestina.
Kwa mujibu wa uchambuzi wa shirika la habari la Al Jazeera, jumla ya waandishi wa habari 278 wameuawa na Israel katika vita vya hivi karibuni vya Ghaza, tarehe 10 Agosti mwaka huu, Israel katika kitendo cha kikatili ilimuua Anas al-Sharif pamoja na waandishi wengine sita.
Chanzo: Asia Pacific Report
Maoni yako