Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuna ya Shirika la Habari la Hawza, Harakati ya Amal kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya kutoweka Imam Sayyid Musa Sadr iliandaa hafla katika mji wa Burj Rahal ambayo ilihudhuriwa na Ali Khreis, mbunge wa Lebanon; Muhammad Ghazal, mwanachama wa ofisi ya kisiasa; Hussein Ma‘ni, msimamizi wa eneo la nne; Qasim Safa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtazamo wa Kitaifa; Dawud Izz al-Din, meya na wajumbe wake; Mukhtar Rabi‘ Khalil, Naibu wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Bara la Afrika; Ma‘ruf Yusuf al-Sahili, mfanyabiashara; Yasin Ghazal, miongoni mwa maafisa wa Harakati ya Amal huko Burj Rahal; pamoja na wanachama wa tawi la harakati hiyo na kikundi cha skauti wa ujumbe wa Kiislamu katika mji huo.
Hafla hii ilianza kwa hotuba ya Mahdi Zalzali, msimamizi wa kitamaduni wa eneo la nne, Kisha Sheikh Hassan Abdullah, Kadhi na Mufti wa Sur na Jabal ‘Amil, alihutubia na kusisitiza kwamba Imam Musa Sadr katika maisha yake aliakisi dhana ya Karbala na njia ya Mitume na Mawalii, alijenga mtazamo wake wa kijamii juu ya msingi wa imani na maelewano, mbali na upendeleo na migogoro.
Sheikh Abdullah alibainisha kwamba changamoto za sasa zinahitaji kushikamana na umoja wa Kiislamu–Kikristo, na kwamba mazungumzo ya kisiasa yanayotegemea upendeleo yanamuhudumia adui Mwisraeli na kuyafanya maisha ya kitaifa kudumaa.
Akasema kuwa umoja wa kitaifa ambao Imam Musa Sadr tangu mwaka 1967 amekuwa akiuombea, bado ni msingi wa kukabiliana na changamoto, na kwamba kuheshimu wingi wa mawazo na mitazamo kunaimarisha uthabiti wa kisiasa.
Maoni yako