Jumanne 2 Septemba 2025 - 18:33
Vijana wengi nchini Marekani, Wanaikingia kifua Palestina

Hawza/ Utafiti mpya na wa kina unaonyesha kwamba idadi kubwa ya rika la vijana, maarufu kama Kizazi cha vijana, nchini Marekani ni wafuasi madhubuti wa Palestina na Ghaza

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, utafiti mpya uliofanywa na Harris Poll na HarrisX mwezi Agosti 2025, ulionyesha kuwa Kizazi cha vijana, katika kujibu swali kwamba: “Katika vita vya Ghaza na Israeli, je, mnaunga mkono Israeli au Hamas?”

Asilimia 60 ya washiriki wa Kizazi cha vijana walijibu kwamba wanaunga mkono kikundi cha Muqawama cha Ghaza, yaani Hamas, aidha, zaidi ya nusu ya washiriki walisema kuwa wanaamini Israeli inatekeleza mauaji ya kimbari huko Ghaza.

Hata hivyo, kwa kuwa vituo hivi vya utafiti viko chini ya udhibiti wa serikali ya Marekani, maswali zaidi kuhusiana na nia ya kuiunga mkono Palestina kwa upana hayakuulizwa.

Lakini tafiti nyingine zilizofanyika hivi karibuni nchini Marekani zinaonyesha kwamba sehemu kubwa ya jamii inaiunga mkono Palestina na inahofia ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Israeli, utafiti wa hivi punde zaidi uliochapishwa na Chuo Kikuu cha Quinnipiac umethibitisha jambo hili.

Ikumbukwe kuwa Israeli katika vita vyake vinavyoendelea dhidi ya Gaza tayari imewaua zaidi ya watu 63,000.

Chanzo: MIDDLE EAST EYE

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha