Jumatano 3 Septemba 2025 - 00:21
Umoja wa Ulamaa wa Muqawama Ulimwenguni: Jinai zinazofanywa na Wazayuni Haziwezi Kudhoofisha Azma ya Taifa la Yemen

Hawza/ Umoja wa Ulamaa wa Muqawama Ulimwenguni, kufuatia shambulizi la anga lililofanywa na  utawala wa Kizayuni lililolenga kikao rasmi cha kiserikali mjini Sana’a, mji mkuu wa Yemen, umetuma salamu za rambirambi na kuonesha mshikamano wake

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Umoja wa Ulamaa wa Muqawama umetuma salamu za rambirambi na mshikamano wake kwa taifa na uongozi wa Yemen, kufuatia shambulizi la anga lililofanywa na utawala wa Kizayuni lililolenga kikao rasmi cha kiserikali mjini Sana’a na kusababisha kuuawa kishahidi mjahid Ahmad Ghalib al-Ruhawi, Waziri Mkuu wa Serikali ya Mabadiliko na Ujenzi, pamoja na mawaziri kadhaa na wenzake waliokuwa naye.

Katika tamko lake, umoja huu umesisitiza kwamba adui wa Kizayuni, kwa kulenga mkutano wa kiraia wa serikali halali iliyokuwa ikisimamia masuala ya nchi na kutoa huduma kwa wananchi wake, umevunja kwa dhahira vigezo vyote vya maadili na kisiasa.

Umoja wa Ulamaa wa Muqawama umesisitiza kuwa: uvamizi huu unakuja katika muktadha wa jitihada za kuvunja azma ya Wayemen na kuwazuia kuendelea kuiunga mkono Ghaza, Palestina na Lebanon.

Tamko hili limeongeza kuwa jinai hii ya Kizayuni, ambayo ni mwendelezo wa mfululizo wa jinai za Israel huko Ghaza, Lebanon na Syria, haitadhoofisha bali itaongeza tu dhamira ya taifa la Yemen kuendeleza mapambano, kusimama imara katika msimamo wao, na kuendeleza msaada wa kivita.

Tamko hili pia limebainisha kuwa Yemen ina uwezo wa kushinda pigo hili, kujaza nafasi ya mashahidi wake, na kuendelea kurusha makombora kuelekea malengo ya Kizayuni katika ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa kimabavu.

Mwisho, Umoja wa Maimamu wa Muqawama umewaombea mashahidi wa Yemen na taifa hilo, kwamba damu yao safi iwe ndio gharama ya ushindi na mlango wa kuelekea uhuru, huku ukisisitiza juu ya kuendeleza jukumu la kubeba amana na kuendelea na njia hadi kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha