Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, kwa mujibu wa simulizi ya tovuti ya habari ya Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya 14 Februari, maeneo mbalimbali ya Bahrain yalishuhudia maandamano ya wananchi wakipinga mapokezi ya balozi mpya wa utawala wa Kizayuni katika mji mkuu wa nchi hii, maandamano haya yalifanyika licha ya kuwepo kwa masharti ya kiusalama na uwepo wa vikosi vya polisi vilivyokusudia kuyazuia.
Katika muktadha huu, wananchi wa maeneo ya Duraz na Karbabad kwa kufanya maandamano, walibeba juu bendera za Bahrain na Palestina kama ishara ya upinzani, na kwa kutoa kauli mbiu walilaani uwepo wa balozi wa Kizayuni katika ardhi ya Bahrain, na vilevile walilaani vita vya kulazimishwa vinavyo endeshwa na utawala wa kigaidi na Marekani dhidi ya nchi za eneo hili.
Waandamanaji walisisitiza mshikamano wao kamili na “mhimili wa mapambano ya Kiislamu” huko Palestina, Yemen, Lebanon na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika maandamano haya ya Karbabad, idadi ya askari wa usalama wa mfumo unaotawala walijaribu kuwatawanya waandamanaji.
Vilevile, kuta za mji wa Shahrakan zilibandikwa kauli mbiu za kimapinduzi dhidi ya mapokezi ya balozi wa Kizayuni na kusisitiza juu ya kuchukia kwa wananchi hatua ya “kudhibiti uhusiano na Israeli.”
Ni jambo la kutajwa kuwa Abdullatif al-Zayani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, siku ya Alhamisi tarehe 6 Shahrivar (28 Agosti) alipokea hati ya utambulisho wa balozi mpya wa utawala wa Kizayuni nchini Bahrain, Shmuel Revel.
Maoni yako