Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, waendesha pikipiki hawa ni wanajumuiya wa kundi lijulikanalo kama Palestina Huru, ambalo linajumuisha waendesha pikipiki kutoka Uholanzi, Ubelgiji na Ujerumani, ambao walifanya maandamano katika njia iliyokuwa ikiishia The Hague.
Waendesha pikipiki walipandisha bendera za Palestina na walivaa shali mabegani mwao, katika njia iliyopangwa kwa ajili ya matembezi haya ya pikipiki, waendesha pikipiki walipita mbele ya maeneo yenye umuhimu mkubwa, mojawapo ikiwa ni Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya The Hague.
Baada ya kukamilika kwa maandamano haya, waendesha pikipiki walirejea katika sehemu ya kuanzia, yaani Uwanja wa Maliwold.
Chanzo: Shirika la Habari la Anadolu
Maoni yako