Jumatano 3 Septemba 2025 - 00:34
Tamko la Pamoja la Wawakilishi wa Ataba Tukufu za Iran Kuhusu Kulaani Jinai iliyofanywa na Utawala wa Kizayuni Nchini Yemen

Hawza/ Kamati ya Wawakilishi wa Ataba Tukufu Iran wamelaani vikali shambulizi la kigaidi, la kinyama na lisilo la haki lililofanywa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya taifa huru na wananchi wajasiri na wenye subira wa Yemen

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, wawakilishi wa Ataba Tukufu za Iran katika tamko lao la pamoja wamelaani jinai za utawala wa Kizayuni katika shambulizi lililolenga Yemen na kuuawa kwa wingi viongozi na wananchi wa nchi hiyo.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

"Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia."
(Haj, Aya 39)

Kamati ya Wawakilishi wa Ataba Tukufu za Iran, kwa mioyo iliyojaa huzuni na kuchukizwa, inalaani vikali shambulizi la kigaidi, la kinyama na lisilo la haki lililofanywa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya taifa huru na wananchi wajasiri na wenye subira wa Yemen, ambalo limehusisha kuuwawa kishahidi na kiheshima Bwana Ahmad Ghalib al-Ruhawi, Waziri Mkuu mtumishi wa kweli, pamoja na mawaziri wengine na viongozi wakuu wa Yemen, kitendo hiki cha kinyama kimeonesha uso mbaya wa adui wa binadamu na wenye kuvunja wazi sheria za Mungu, haki za kimataifa na heshima ya binadamu.

Mapambano yenye ujasiri ya wananchi wa Yemen katika kulinda misingi ya Palestina na kuwaunga mkono wananchi Madhulumu wa Ghaza ni jukumu la kiimani na la kibinadamu, ambalo leo linaigharimu damu safi ya wapendwa wao, Msimamo huu, mbele za Mwenyezi Mungu Mwenye Uwezo, utazalisha thawabu kubwa na ushindi wa mwisho.

Hakika, jinai hii mbaya iliyofanywa na kundi la Kizayuni na madai yao ya uongo ya ustaarabu na haki za binadamu inaonyesha kina cha uharibifu wa maadili na kutojali kabisa mafundisho ya dini za Mwenyezi Mungu, kanuni za msingi za haki za binadamu, na mikataba yote ya kimataifa, hasa Mikataba ya Geneva na Katiba ya Umoja wa Mataifa.

Kamati ya Wawakilishi wa Ataba Tukufu na Mahali patakatifu za Iran, kwa kutoa rambirambi zake za dhati kwa taifa jasiri la Yemen, serikali halali ya nchi hiyo, na familia zilizopoteza wapendwa wao, inahimiza jumuiya ya kimataifa, mashirika yanayohusika ya kimataifa, na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuchukua hatua za dhati na za kivitendo dhidi ya uvamizi huu wa wazi, ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, na jinai za kibinadamu, na kuhakikisha ufuatiliaji wa kisheria na adhabu kwa waamuru na watendaji wa jinai hii ya kigaidi.

Tunawaomba pia nchi zote huru, wanasayansi, watetezi wa haki za binadamu na wenye dhamira safi duniani kote, kuchukua msimamo wenye uwajibikaji dhidi ya ujinga huu na uvamizi wa wazi, na kwa vitendo kuzuia kurudiwa kwa jinai kama hizi za kutisha, na kusisitiza umuhimu wa kufuata haki za kibinadamu, haki za mataifa, Katiba ya Umoja wa Mataifa, na kanuni za lazima za sheria ya kimataifa.

Kamati ya Wawakilishi wa Ataba Tukufu na Mahali patakatifu za Iran zinathibitisha tena kwa nguvu na kwa ukamilifu msaada wake kwa taifa jasiri na madhulumu la Yemen, na kusisitiza haki halali na isiyovunjika ka wananchi wa nchi hii kulinda uhuru, mipaka ya taifa na heshima ya kibinadamu kwa msaada wa fadhila za Mwenyezi Mungu.

Wawakilishi wa Ataba Tukufu za Iran:

Ataba Tukufu ya Razavi

Ataba Tukufu ya Bibi Fatima Masumah (as)

Ataba Tukufu ya Ahmad bin Musa al-Kazim (as)

Ataba Tukufu ya Abdul Azim Hasani (as)

Msikiti Mtakatifu wa Jamkaran
Shirika la Waqf na Mambo ya Hisani la Nchi

Wakala wa Wilayatul Faqih kwa Masuala ya Hajj na Ziara

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha