Jumatano 3 Septemba 2025 - 07:11
Umuhimu wa kuimarisha mtazamo wa kimataifa wa Hawza / Hawza zinapaswa kuwa na nafasi yenye athari katika uwanja wa kimataifa

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, huku akisisitiza juu ya umuhimu wa uwepo wa kina na wa kivitendo wa Hawza katika uwanja wa kimataifa, amesema: uzalishaji wa kielimu unaolingana na lugha na mtazamo wa kimataifa pamoja na mipangilio iliyopangwa kwa utaratibu, ni miongoni mwa vipaumbele vya kimsingi vya Hawza ili kuongeza athari zake katika kiwango cha kimataifa na vilevile kitaifa

Kwa mujibu wa mwandishi wa  Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawza za kielimu nchini Iran, katika kikao na Baraza la Wakurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Hawza, akitoa ripoti ya ushiriki wake katika kongamano la pili la kimataifa la viongozi wa kidini lililokuwa na mada ya “Nafasi ya viongozi wa kidini katika kutatua mizozo ya kibinadamu” lililofanyika nchini Malaysia, alisema: Tulihudhuria Malaysia kwa muda wa siku tatu; Jumatano, Alhamisi na Ijumaa, na katika muda huo kulifanyika programu mbalimbali ambazo nitazigusia kwa jumla.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza za kielimu ameongeza: Miongoni mwa programu hizo kulikuwa na kikao na Jumuiya ya wahitimu wa Hawza, ambapo kikao hicho tulijadili masuala ya kielimu, kiutamaduni na Kiislamu nchini Malaysia. Mapendekezo kuhusu shughuli za kiutamaduni na kimadhehebu yalitolewa, na kusisitizwa juu ya kuinua kiwango cha elimu pamoja na kuzingatia umoja na maslahi ya Uislamu na nchi ya Malaysia.

Mkurugenzi wa Hawza vilevile ameeleza juu ya kikao na baadhi ya maulamaa, wanafikra na wasomi wa Malaysia ambapo mijadala muhimu ilifanyika na kubadilishana mawazo, mada zilizohusu masuala ya kikanda na kidini zilijadiliwa, waliokuwepo walilisifu msimamo wa mfumo wa Kiislamu wa Iran dhidi ya Israel na wakatoa mawazo na mapendekezo yao.

Ayatullah A‘rafi amebainisha: Kuhusu upeo wa mkutano huo uliokuwa lengo kuu la safari, ilibainishwa kuwa takribani wanazuoni, wasomi na wanafikra elfu moja kutoka nchi 54 tofauti na pia wawakilishi wa dini nyingine akiwemo Wakristo na Wabudha walihudhuria.

Mkurugenzi wa Hawza za kielimu nchini, akibainisha umuhimu wa mada zilizojadiliwa kwenye mkutano huo, alisema: Imesisitizwa kwamba maulamaa wana majukumu mawili; la kwanza, kuleta umoja ndani ya madhehebu, kati ya umma wa Kiislamu, na hata zaidi ya hapo baina ya dini mbalimbali; na la pili, kupambana na dhulma na kudai haki, majukumu haya mawili ndio msingi wa kazi za maulamaa, na mtazamo wa Mapinduzi ya Kiislamu unasisitiza hayo katika uwanja wa kimataifa.

Ayatullah A‘rafi amesema: Kuhusu suala la Ghaza pia, ilisisitizwa kuwa  uthabiti na ustahimilivu wa watu wa Ghaza na mhimili wa muqawama kwa upande mmoja, na kuanguka kwa maadili na dhulma isiyo na kikomo ya Wazayuni kwa upande mwingine, ni nyuso mbili kwenye sarafu moja, Msimamo wetu kuhusu utawala wa kandamizi katika nchi tofauti; sisi hatutambui kamwe serikali ambazo hazijaundwa kwa uchaguzi wa kweli, bali tunatambua kukubali uchaguzi wa Wapalestina, na kinyume chake tunachukulia muqawama na jihad ya kweli kuwa msingi, Katika mkutano huu madai manane yaliwasilishwa ambayo yanapaswa kufuatiliwa kwa umakini.

Ayatullah A‘rafi ameendelea kusema: Pembeni mwa mkutano huu, kulifanyika pia vikao kadhaa na viongozi wa Malaysia, Saudi Arabia, Misri na baadhi ya vyama na harakati za Kimalaysia, vikao hivyo vilikuwa fursa nzuri ya kubadilishana mawazo juu ya mabadiliko ya kielimu, ya Hawza na ya kidini ya Iran.

Mkurugenzi wa Hawza za kielimu nchini Iran, akisisitiza juu ya umuhimu wa umoja wa Kiislamu na mijadala ya pamoja ya kifiqhi na kifalsafa na maulamaa mbalimbali, amesema: Ni lazima tutegemee mambo ya pamoja ili kuimarisha zaidi umoja na mshikamano, na vilevile kubainisha misimamo yetu na mtazamo wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatullah A‘rafi katika maelezo yake kuhusu mabadiliko ya kimtazamo katika eneo na nafasi ya Hawza amesema: Mabadiliko ya mitazamo ya taasisi kama Rabita al-‘Alam ni fursa kwa ajili yetu, na bila shaka hatupaswi kughafilika na ukuaji wa mtazamo wa kisekula na mielekeo ya Kimagharibi.

Umuhimu wa kuimarisha mawasiliano baina ya maulamaa na taasisi za kidini

Ayatullah A‘rafi, akibainisha umuhimu wa kuimarisha mawasiliano kati ya maulamaa na taasisi za kidini, amesema: Katika safari hii tuliona kwamba Waziri Mkuu wa Malaysia na wajumbe wengine wa ujumbe wa Iran walijenga uhusiano mzuri sana, na hii ilikuwa fursa ya kushirikiana zaidi.

Amesisitiza: Hawza katika mazingira mapya lazima izidi kuelekea kwenye kujenga mitazamo na kuzalisha fasihi ya kifikra, kwa sababu udhaifu mkubwa unahisiwa katika nyanja hii, na Hawza, kama taasisi ya kidini na kielimu, inapaswa kuwa kinara wa kuzalisha na kusambaza maudhui na fikra za Uislamu Safi na kuwa na nafasi kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Mkurugenzi wa Hawza za kielimu nchini Iran ameongeza: Tuna tafiti nyingi na walimu mashuhuri katika masuala ya K‘alam, Fiqhi, Hadith, Tafsiri na sayansi za kibinadamu ndani ya Hawza, lakini kujitokeza na kushiriki kwa kina katika vyombo vya habari na uwanja wa kimataifa bado kunahitaji juhudi zaidi. Ni lazima tujitambulishe vizuri zaidi, na mageuzi ya kielimu na kifiqhi ya Iran yaonekane na yasikike zaidi katika kiwango cha kimataifa, Hawza lazima ishughulikie zaidi kushiriki katika majukwaa ya kimataifa, bila shaka, kuwasilisha na kueneza fikra tukufu za Uislamu na elimu ya Ahlul-Bayt (‘a) pamoja na sayansi ya Kiislamu kwa upana wake wote, kunahitaji upangaji upya na uwekezaji makini unaoendana na mazingira ya kimataifa, na hapa ndipo tunapokuwa na udhaifu na inahitajika juhudi za dhati.

Ayatullah A‘rafi amegusia pia umuhimu wa kuzingatia mabadiliko mapya katika siasa za baadhi ya nchi na amesema: Mabadiliko haya ni fursa kubwa lakini pia ni tishio kubwa, na iwapo hatutaweza kusimamia kwa usahihi mipangilio na siasa zetu, tutapoteza mambo mengi, kwani wao wanakwenda kwa kasi na kuweka nafasi ya Iran kwenye changamoto.

Vilevile amesisitiza kwamba uhusiano wa Iran na Malaysia ni thabiti, na jambo hili limeisaidia nafasi na athari ya ujumbe wa Iran katika kongamano, msimamo wa Mapinduzi ya Kiislamu uliwasilishwa vyema katika mkutano huu, Hawza za kielimu zinapaswa kuongeza zaidi uwepo wake wa kimataifa na athari zake, na jambo hili ni miongoni mwa masuala ya msingi ya wakati huu kwa Hawza.

Vilevile amebainisha suala muhimu la kujitambulisha kwa Hawza katika ulimwengu: Kwa masikitiko, Hawza za kielimu za Iran hazijulikani vya kutosha katika kiwango cha kimataifa, na maarifa na uelewa kuhusu Hawza ni kidogo, baadhi ya taasisi pia hazina uwezo wa kutosha kwa ajili ya kujenga mitazamo na kushiriki katika uwanja wa kielimu na kifikra wa kimataifa, tatizo hili limekuwepo tangu miaka mingi iliyopita, na ili kuendeleza na kuathiri ni lazima kuwe na uwekezaji na mipangilio thabiti.

Umuhimu wa kuimarisha mtazamo wa kimataifa wa Hawza/ Hawza lazima ijulikane ulimwenguni

Mkurugenzi wa Hawza za kielimu nchini Iran, akisisitiza juu ya umuhimu wa uwepo wa kina na wa kivitendo wa Hawza katika uwanja wa kimataifa, amesema kwamba uzalishaji wa kielimu unaolingana na lugha na mtazamo wa kimataifa pamoja na mipangilio ya kimaandalizi, ni miongoni mwa vipaumbele vya kimsingi vya Hawza ili kuongeza athari zake katika kiwango cha dunia na vilevile ndani ya nchi, Hawza lazima ichukue nafasi katika uwanja wa kimataifa.

Ayatullah A‘rafi amesisitiza: Waislamu ulimwenguni kwa sasa wako katika hali ya wasiwasi mkubwa na kuna haja ya dharura ya mtazamo wa kimataifa na uwepo wa kina wa Hawza katika uwanja wa kimataifa, tuna nadharia sahihi na za kina lakini katika kuzilinganishisha na fasihi ya kimataifa na mtazamo wa kulinganisha na madhehebu mengine bado tuna udhaifu, kwa mfano, inatupasa tuweze kuwasilisha nadharia zetu katika K‘alam, Fiqhi na Tafsiri sambamba na nadharia za Ahlus-Sunna au madhehebu mengine kwa mtazamo wa kulinganisha. Mafanikio haya katika Usul na Fiqhi na nyanja zingine ni yenye thamani kubwa, na yakijulikana ipasavyo yanaweza kuwa na athari kubwa.

Vilevile amesema: Taasisi za Hawza lazima zielekee kwenye uzalishaji wa maudhui ya kulinganisha, ya kiutendaji na ubunifu wa kielimu kuelekea kutoa mtazamo wa kimataifa, jambo hili linahitaji katiba na mpango wa kitaifa uliothibitishwa na kutekelezwa, amepongeza jitihada zilizoanza katika uwanja huu, lakini amesisitiza kuwa hazitoshi, na kwamba ni lazima kazi za msingi na zilizo na uratibu zaidi zifanyike, na imeamuliwa kuandaliwa mpango wa jumla.

Ayatullah A‘rafi, akihitimisha kwa kubainisha umuhimu wa suala hili, amesema: Pindi Hawza zitakapojulikana duniani na kuwa na mitazamo yenye nguvu na yenye athari, nafasi hiyo ya kimataifa italeta matokeo chanya ya ndani, ikiwemo katika siasa, uchumi na utamaduni wa nchi. Hawza inapaswa kutumia fursa hizi na kwa kupanga na jitihada kubwa, kuwasilisha mtazamo wa Kiislamu ulimwenguni.

Mwisho wa ujumbe

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha