Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Dkt. Smith, baada ya kumfanyia uchunguzi wa kitabibu Bw. Khalid, alithibitisha hali mbaya sana ya mwili wake na kuanza kudhoofika viungo vyake vya ndani. Alisema kuwa timu ya kisheria inayoshughulikia masuala ya wafungwa wanaofanya mgomo wa kula sasa ina ushahidi mzito unaoweza kutumiwa katika uchunguzi kuhusu madai ya manyanyaso yaliyofanywa dhidi ya mfungwa huyo.
Aliongeza kuwa: “Bw. Muhammad Omar Khalid kwa sasa yuko karibu kupata mshtuko wa moyo. Endapo ataamua kusitisha mgomo wake wa kula, hataweza kula kama kawaida mara moja, kwani hali hiyo inaweza kuhatarisha maisha yake. Badala yake, anahitaji mpango wa lishe ya taratibu chini ya uangalizi wa madaktari, ambao utachukua muda hadi mwili wake uanze kupona kutoka katika udhaifu huu hatari.”
Kwa masikitiko makubwa, utawala wa Uingereza hauoneshi kujali hali ya wafungwa. Mfungwa huyu Muislamu amefungwa gerezani kwa sababu pekee ya kuwaunga mkono watu wa Ghaza na Palestina, na licha ya kufanya mgomo wa kula, hata haki za msingi kabisa zinazotambuliwa kimataifa kwa wafungwa wanaogoma kula hazikuzingatiwa katika magereza ya utawala wa Uingereza.
Chanzo: Imenukuliwa kutoka 5Pillars
Maoni yako