Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Simon Harris alisisitiza kuwa kuzingirwa kunakoendelea Ghaza, sambamba na uharibifu wa miundombinu na uhaba wa mahitaji ya msingi ya kibinadamu, kumesababisha hali mbaya kupita kiasi ambayo imeathiri kwa kiwango kikubwa mamia ya maelfu ya wakazi, hususan makundi yaliyo katika mazingira magumu kama watoto, wazee na wagonjwa wanaohitaji huduma za matibabu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland alisema katika taarifa yake: “Hali ya Ghaza ni ya dharura. Hatari ya kutokea kwa njaa ipo, isipokuwa hatua za haraka zichukuliwe ili kuruhusu uwasilishwaji wa kweli wa chakula, maji, dawa na misaada mingine muhimu.”
Aidha, aliitaka jumuiya ya kimataifa, nchi zinazohusika na misaada kwa Ghaza, mashirika ya kimataifa pamoja na taasisi za misaada ya kibinadamu kuongeza kwa dhati ufadhili na msaada wa vifaa (lojistiki) ili kuzuia kuzidi kudorora kwa hali ya maisha huko Ghaza. Alisisitiza kuwa; upatikanaji endelevu wa misaada ya kibinadamu si wajibu wa kimaadili pekee, bali pia ni wajibu wa kisheria chini ya sheria za kimataifa.
Kauli hizi zimetolewa wakati ripoti zinaendelea kuongezeka kuhusu uhaba mkubwa wa chakula, utapiamlo ulioenea kwa kiwango kikubwa, na upungufu mkali wa vifaa vya tiba katika Ukanda wa Ghaza, huku wananchi wa Palestina wakiendelea kuteseka kutokana na athari za mzozo wa muda mrefu na uwasilishaji mdogo sana wa misaada ya kibinadamu.
Chanzo: EUPAC
Maoni yako