Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Habari za Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, siku ya Jumapili tarehe 9 Shahriwar, wawakilishi kutoka nchi 45 za dunia walikusanyika nchini Tunisia kwa dhumuni la kupanda kwenye makumi ya meli na kuanza safari yenye hatari kuelekea Ghaza, lengo la msafara huu wa kimataifa ni kufikisha misaada ya kibinadamu na kuondosha mzingiro wa eneo hili.
Licha ya vitisho vya wazi kutoka kwenye utawala wa Kizayuni kuhusiana na kuwakamata au kuwaua mshiriki yeyote wa harakati hii, wanaume na wanawake waliomo kwenye msafara huu, kwa dhima ya kibinadamu na iliyo juu ya mipaka ya kitaifa na kidini, wameweka maisha yao rehani ili kufikisha ujumbe wa amani na uadilifu.
Miongoni mwa waliojitolea wapo watu wa dini na mataifa mbalimbali, likiwepo pia kundi la wanaharakati na makundi ya kijamii kutoka Iran, jambo linaloashiria mshikamano wa kimataifa na wananchi waliodhilumiwa wa Ghaza na upinzani dhidi ya mauaji ya kimbari na vizuizi.
Kwa mujibu wa mipango iliyowekwa, msafara huu wa kibinadamu wa majini utaondoka bandarini Tunisia kuelekea Ghaza ndani ya siku tatu zijazo, harakati hii inaweza kubadilika na kuwa alama yenye nguvu ya kusimama kwa dhamira ya dunia dhidi ya dhulma na ukosefu wa haki.
Ujumbe ulio wazi wa harakati hii ya kimataifa ni huu:
“Ghaza haiko peke yake, na hata tishio la kifo haliwezi kuizuia irada ya watu huru duniani kwenye kuwatetea watu waliodhulumiwa.”
Maoni yako