Jumanne 10 Juni 2025 - 22:02
Baadhi ya Sifa za Kurejea Duniani (raj'a)

Hawza/ Kwa waumini wote na wanaosubiri kwa dhati kudhihiri kwa Imam Mahdi (as), ambao wamefariki kabla ya kudhihiri kwake, kuna uwezekano wa kurudi duniani na kumsaidia Imam huyo.

Shirika la Habari la Hawza | Kutokana na riwaya nyingi zilizopokelewa, mambo haya yafuatayo yanaweza kusemwa kuhusu kurejea duniani (Raj'a):

1. Raj'a ni miongoni mwa siku kubwa na muhimu ulimwenguni, ambazo zimeitwa “Ayāmullāh” [Siku za Mwenyezi Mungu].

Imam Swādiq (as) amesema kuhusu hili:

«أَیَّامُ اللَّهِ ثَلاَثَةٌ: یَوْمٌ یَقُومُ الْقَائِمُ علیه‌السلام، وَ یَوْمُ الْکَرَّةِ، وَ یَوْمُ الْقِیَامَةِ.»

“Ayyāmullāh” siku za Mwenyezimungu ni tatu: Siku ya kusimama al-Qā’im as, siku ya kurudi duniani, na siku ya Kiyama. (Bihār al-Anwār, juzuu ya 53, uk. 63)

2. Kuamini kurudi duniani (Raj'a) ni miongoni mwa alama za Wafuasi wa Ahlul-Bayt as.

Imam Swādiq (as) amesema:

«لَیْسَ مِنَّا مَنْ لَمْ یُؤْمِنْ بِکَرَّتِنَا.»

Yule asiyeamini katika kurudi kwetu duniani (Rj'a) si miongoni mwetu. (Bihār al-Anwār, juzuu ya 53, uk. 92)

3. Raj'a si jambo la jumla kwa watu wote; kama ambavyo Imam Swādiq (as) amesema:

«إِنَّ الرَّجْعَةَ لَیْسَتْ بِعَامَّةٍ، وَ هِیَ خَاصَّةٌ، لَا یَرْجِعُ إِلَّا مَنْ مَحَضَ الْإِیمَانَ مَحْضاً، أَوْ مَحَضَ الشِّرْکَ مَحْضاً.»

Kurudi duniani si kwa wote, bali ni kwa wale tu waliotakasika kabisa kwa imani safi au wale waliokuwa katika shirki ya wazi wazi. (Bihār al-Anwār, juzuu ya 53, uk. 39)

4. Miongoni mwa waumini watakaorudi duniani ni Mitume na Maimamu Maasumu (as), na Imam wa kwanza atakayehakikisha uongozi wa uadilifu wa kimataifa baada ya Imam Mahdi as katika zama za kurudi duniani, ni Imam Hussein (as), ambaye atatawala kwa miaka mingi, Imam Swādiq as amesema:

«أَوَّلُ مَنْ یَرْجِعُ إِلَى الدُّنْیَا الْحُسَیْنُ بْنُ عَلِیٍّ علیه‌السلام، فَیَمْلِکُ حَتَّى یَسْقُطَ حَاجِبَاهُ.»

Mtu wa kwanza atakayerudi duniani ni Hussein bin Ali (as), na atatawala mpaka nyusi zake zianguke juu ya macho yake kwa sababu ya uzee. (Bihār al-Anwār, juzuu ya 53, uk. 46)

5. Kwa waumini wote na wanaosubiri kwa dhati kudhihiri kwa Imam Mahdi (as) ambao walifariki kabla ya kudhihiri kwake, kuna uwezekano wa kurudishwa duniani ili wamsaidie Imam huyo.

Imepokewa kutoka kwa Imam Swādiq (as) kuwa kila mtu atakayesoma dua ya ahadi (دعاء العهد) kwa muda wa asubuhi arobaini mfululizo, atakuwa miongoni mwa wasaidizi wa Qa'im wetu (as). Na ikiwa atafariki kabla ya kudhihiri kwa Imam huyo, basi Mwenyezi Mungu atamfufua kutoka kaburini ili awe katika huduma ya Imam Mahdi (as).
(Mafātīḥ al-Jinān, katika utangulizi wa Du‘ā al-‘Ahd)

Sehemu ya Du‘ā al-‘Ahd:

«... اللَّهُمَّ إِنْ حَالَ بَیْنِی وَ بَیْنَهُ الْمَوْتُ الَّذِی جَعَلْتَهُ عَلَىٰ عِبَادِکَ حَتْماً مَقْضِیّاً، فَأَخْرِجْنِی مِنْ قَبْرِی ...»

Ee Mwenyezi Mungu! Ikiwa kifo ambacho umekifanya kuwa hakika isiyoepukika kwa waja wako kitanizuia mimi na yeye (Imam Mahdi as), basi nifufue kutoka kaburini nikiwa nimevikwa sanda. (Mafātīḥ al-Jinān; Bihār al-Anwār, juzuu ya 99, uk. 111)

6. Makafiri na wanafiki hawatarudi duniani kwa hiari yao, bali watalazimika kurejea kwa kulazimishwa, lakini kurudi kwa waumini kunatazamiwa kuwa kwa hiari.

Imam Swādiq (as) amesema:

«إِذَا قَامَ، أُتِیَ الْمُؤْمِنُ فِی قَبْرِهِ، فَیُقَالُ لَهُ: یَا هَذَا! إِنَّهُ قَدْ ظَهَرَ صَاحِبُکَ، فَإِنْ تَشَأْ أَنْ تَلْحَقَ بِهِ فَالْحَقْ، وَ إِنْ تَشَأْ أَنْ تُقِیمَ فِی کَرَامَةِ رَبِّکَ فَأَقِمْ.»

Imam Mahdi as atakapodhihiri, malaika wa Mwenyezi Mungu watawasiliana na waumini waliomo makaburini na kuwaambia: Ewe mja wa Mwenyezi Mungu! Bwana wako amedhihiri. Ikiwa unataka kuungana naye, fanya hivyo; na ikiwa unataka kubaki katika neema za Mola wako (katika ulimwengu wa barzakh), basi endelea kubaki. (al-Ghayba, Shaykh Ṭūsī, juzuu ya ۱, uk. 458)

Utafiti huu unaendelea…

Imenukuliwa kutoka katika kitabu “Negin-e Āfarinish” huku ikifanyiwa marekebisho kiasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha