Jumapili 31 Mei 2026 - 15:20
Mwakilishi wa Hizbullah: Muqawama utaivuruga mipango ya Israel

Hawza/ Hassan Fadhlallah, mwakilishi wa Harakati ya Uaminifu kwa Muqawama wa Hizbullah, alisisitiza kwamba; adui Israeli inaendelea kutekeleza mashambulizi yanayoongezeka kusini mwa Lebanon na akaelezea makabiliano haya kuwa ni vita vya kusalia na kusimama imara.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mwakilishi wa Hizbullah katika hotuba yake kwenye hafla ya kumbukumbu ya shahidi mujahid Hussein Ghassan Fawaz, iliyokuwa ikiandaliwa na Hizbullah, alisisitiza kuwa: "Tunakabiliwa na uvamizi wa umwagaji damu kutoka kwa utawala wa kinyama wa Israel ambao lengo lake ni kuikalia ardhi yetu na kutufukuza, hatuna chaguo jingine isipokuwa kuhuisha muqawama na kusimama imara."

Aliongeza kwamba; wapiganaji wa muqawama wa Lebanon "wanaandika simulizi za kishujaa ardhini", wakati kukiwa na kutokuwapo uwiano katika baadhi ya masuala ya kijeshi.

Aliongeza kwa kusema: “Muqawama haufanyi kazi kama jeshi la kawaida kwa ajili ya vita vya mipakani, bali badala yake unajitahidi kuhakikisha uwepo wa kudumu wa majeshi ya Israel kuwa jambo lisilowezekana kwa utawala huo.”

Kazi ya muqawama kwa hakika ni kuzuia kuanzishwa kwa vituo vya kijeshi na utawala wa Kizayuni pamoja na kudhoofisha nguvu zake kupitia operesheni mbalimbali.

Alisema kwamba; hata kama majeshi ya Israel yataingia katika vijiji vya mpakani, yatakabiliwa na ipasavyo.

Hassan Fadlallah alionya kwamba; wananchi wa muqawama wa Lebanon "wanalipa gharama kubwa kwa damu na mali zao", na akaongeza: "Sisi si watu wa kupenda vita, bali tunatafuta maisha yenye heshima."

Pia alieleza kuwa uchaguzi ulio mbele ya Lebanon kwa sasa una njia mbili: "Kusalimu amri au vita na muqawama." Na akasisitiza kuwa; muqawama ndiyo njia ambayo itaendelea kwa gharama yoyote ile, kauli hii imetolewa kwa mujibu wa ripoti za idara ya mahusiano ya umma ya Hizbullah na imekuwa ikithibitishwa mara kwa mara.

Chanzo: Al-Manar

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha