Jumanne 3 Juni 2025 - 18:08
Kukubalika na umma Imam Mahdi (a.s.) pamoja na Serikali yake

Hawza/ Miongoni mwa sifa za msingi za serikali ya Imam Mahdi (a.s.) ni kuwa serikali hiyo itakubalika na watu wote na jamii zote za kibinadamu. Si tu watu wote wa ardhini, bali hata wakaazi wa mbinguni wataridhika kikamilifu na serikali hiyo ya kimungu na mtawala wake mueneza haki.

Shirika la Habari la Hawza - Moja ya changamoto kuu za serikali mbalimbali imekuwa ni kupata ridhaa ya umma, lakini kutokana na udhaifu mwingi uliokuwemo katika uendeshaji wa jamii, ridhaa hiyo haijawahi kupatikana kikamilifu.

Hata hivyo, miongoni mwa sifa za msingi za serikali ya Imam Mahdi as ni kuwa itakubalika na watu wote na jamii zote za kibinadamu. Si tu wakaazi wote wa ardhi, bali hata wakaazi wa mbingu pia wana ridhaa kamili na serikali hiyo ya kimungu na mtawala wake muadilifu.

Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w) amesema kuhusu jambo hili:

«أُبَشِّرُکُمْ بِالْمَهْدِیِّ یُبْعَثُ فِی أُمَّتِی عَلَی اخْتِلاَفٍ مِنَ اَلنَّاسِ وَ زِلْزَالٍ یَمْلَأُ اَلْأَرْضَ عَدْلاً وَقِسْطاً کَمَا مُلِئَتْ جَوْراً وَظُلْماً یَرْضَی عَنْهُ سَاکِنُ اَلسَّمَاءِ وَسَاکِنُ اَلْأَرْضِ.»

“Nawapeni bishara ya kuja kwa Mahdi (as), atatumwa katika umma wangu wakati watu watakapokuwa katika hali ya mfarakano na misukosuko. Ataijaza ardhi uadilifu na usawa kama ambavyo ilijaa dhulma na uonevu. Na wakaazi wa mbinguni na ardhi wataridhika naye.” (al-Ghaybah ya Shaykh Tusi, Juz. 1, uk. 178)

Na katika riwaya nyingine kutoka kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w) kuhusu Imam Mahdi (a.s), amesema hivi:

«تَأْوِی إِلَیْهِ أُمَّتُهُ کَمَا تَأْوِی اَلنَّحْلُ إِلَی‌ یَعْسُوبِهَا.»

Utamkimbilia yeye kwa hifadhi umma wake, kama vile nyuki wanavyomkimbilia malkia wao kwa hifadhi.” (al-Tashrīf bil-Minan fi al-Taʿrīf bil-Fitan, Juz. 1, uk. 147)

Utafiti huu unaendelea…

Imenukuliwa kutoka katika kitabu cha "Negin-e Afarinish" huku ikifanyiwa marekebisho kiasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha