Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, katika khutba ya Swala ya Ijumaa iliyofanyika katika Husainia ya Fatimiyya mjini Najaf Ashraf, alitahadharisha kuhusu njama inayopangwa dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini Iraq na akasema: Kwa nini Marekani inasisitiza kuvunjwa kwa Harakati ya Hashdu al-Sha’abi, lakini haizingatii kuvunjwa kwa Daesh (ISIS) na Jabhat al-Nusra? Kwa nini inaelekeza mashambulizi yake dhidi ya Hashdu al-Sha’abi, Hizbullah, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), na Ansarullah ya Yemen?
Aliongezea kwa kusema: Kwanza, matamshi haya ni kuingilia mambo ya ndani ya Iraq, na pili, Hashd al-Sha’abi ni mkono wa nguvu wa taifa la Iraq.
Imam wa Ijumaa wa Najaf Ashraf aliendelea kusema kuwa: Serikali pekee haina uwezo wa kuzuia hatari zilizopo, kwa hivyo Harakati ya Hashdu al-Sha’abi ni sehemu rasmi ya ulinzi wa serikali na ni nguvu muhimu kwa taifa.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi pia katika sehemu nyingine ya khutba yake aligusia kuhusiana na matukio ya moto yaliyotokea mara kadhaa mjini Najaf Ashraf kutokana na joto kali, akasema: Mataifa ya ulinzi wa kiraia yalikuwa na mchango mkubwa katika kuzima moto huo. Mungu awarehemu na awape malipo mema, kwani wao ni askari wasiojulikana kwa kazi zao hizi adhimu. Hapa, napenda kutoa shukrani zangu kwa maafisa wetu wa ulinzi wa kiraia kutonana na juhudi zao hizo.
Maoni yako