Jumamosi 31 Mei 2025 - 09:15
Benedict Cumberbatch aungana na waandamanaji dhidi ya mauzo ya silaha kwa Israel

Hawza/ Zaidi ya wasanii 300, madaktari, na wanajumuiya wa chuo kikuu nchini Uingereza, wametia saini barua ambayo inamtaka Waziri Mkuu wa Uingereza kuchukua hatua za haraka kuhusiana na vita vya Ghaza vile vile kusitisha mapigano moja kwa moja.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, watu wa Uingereza wameendeleza upinzani wao dhidi ya mauzo ya silaha yanayo endelea. Katika hili, sura mashuhuri za Uingereza kama Benedict Cumberbatch, mwigizaji wa uingereza, pia amemwomba Waziri Mkuu kusitisha mauzo ya silaha kwa Israel.

Zaidi ya wasanii 300 wakiwemo madaktari na wanachuo wa Uingereza, wametia saini barua na kumtaka Waziri Mkuu aache kushirikiana na Israel, katika barua hiyo imeandikwa: "Tunakuomba uchukue hatua za haraka ili kumaliza hofu na machafuko huko Ghaza."

"Kwa kushirikiana Uingereza na Israel, vurugu pia zinachukua nafasi katika nchi yetu. Vipuri vya ndege na silaha zinazotumwa kutoka viwanda vya Uingereza kwenda Israel, familia zisizo na makazi zinauwawa ndani ya sekunde chache, kuuza kila silaha kunaifanya nchi yetu kuchafua mikono yake moja kwa moja na damu ya watu hawa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha