Ijumaa 16 Mei 2025 - 11:02
Taarifa ya Hawza Kuhusiana na Kauli za dhihaka za Trump / Serikali za ukanda huu zisiingie katika mitego ya upuuzi Huo

Uongozi wa hawza, sambamba na kulaani upuuzi wa Rais mwenye dhalili wa Marekani — ambao umetolewa kwa nia ya kuiunga mkono serikali ya Kizayuni na kuchochea mifarakano baina ya nchi za Kiislamu — unazitaka serikali za ukanda huu kuupa kipaumbele mshikamano katika ukanda huu na kuutazama kwa jicho la pekee mgogoro wa Ghaza, ili zisiruhusu utekelezaji wa malengo ya kibeberu ya Marekani katika eneo hili.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya taarifa ya Kituo cha Usimamizi wa Hawza kuhusiana na matamshi ya dhihaka ya Rais wa Marekani ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Kauli za hivi karibuni za Rais wa Marekani kuhusu Iran — mbazo zililenga kuibua mifarakano kati ya Jamhuri ya Kiislamu na nchi za ukanda huu — zimeonyesha wazi kuwa mkakati wa kuchochea mifarakano na fitina katika eneo hili umewekwa katika ajenda ya serikali ya Marekani.

Ingawa yale aliyoyasema Bwana Trump hayana thamani wala uzito wa kisiasa, na yamedhihirisha kwamba washauri wake wamemfikishia taarifa zisizo sahihi kuhusu Iran, hata hivyo, haya yanatoa haki kwa idara ya diplomasia kuanzisha hatua za kisheria na kimataifa za kulaani matamshi hayo.

Leo hii, Iran, licha ya mashinikizo na vikwazo vyote, imegeuka kuwa miongoni mwa nguvu kuu zisizoweza kupuuzwa katika dunia na eneo hili, na katika njia ya maendeleo na kujitegemea, imejiegemeza juu ya misingi yake imara, na imejivua kabisa minyororo ya utegemezi na tamaa kwa madola ya kimabavu duniani.

Iwapo Jamhuri ya Kiislamu tangia mwanzo wa Mapinduzi imekuwa ikiunga mkono lengo la Palestina na ukombozi wa Quds tukufu, hilo limetokana na uamuzi wa akili, amri ya dini, na haki za kibinadamu. Na leo hii zaidi ya siku nyingine yoyote, imekuwa wazi kuwa lau mataifa ya Kiislamu yangelichukua hatua tangu awali dhidi ya donda hili la saratani, basi leo hii tusingeshuhudia mauaji haya na uhalifu mkubwa dhidi kwa watu wa Ghaza.

Ni Jamhuri ya Irani ambayo hadi sasa imekuwa ikilinda mipaka ya uhuru, heshima, na hadhi ya Wairani, na imekuwa ikijiamini, uwezo wa ndani, na kujitegemea. Na licha ya uadui na njama zote, imezidi kusonga mbele kimaendeleo.

Ni taifa la Iran ambalo, licha ya kuwa mwathirika mkuu wa ugaidi, limekuwa mpambanaji thabiti zaidi dhidi ya ugaidi huo, na katika njia hiyo limepoteza mashahidi wengi. Hata hivyo, kwa masikitiko makubwa, inapaswa kusemwa kuwa Bwana Trump, kwa kuamuru kuuawa kwa shujaa wa mapambano dhidi ya ugaidi wa Daesh—Shahidi Haj Qasem Soleimani—amefichua uso wake wa kweli kiasi kwamba hawezi tena kujitambulisha kuwa mpigania amani wa ukanda huu. Maana kama angelikuwa mkweli katika madai hayo, basi alipaswa kukatisha misaada yake kwa utawala wa Kizayuni unaoua watoto, ili watoto, wanawake na wagonjwa wasiendelee kumwaga damu kwa dhulma.

Uongozi wa hawza, sambamba na kulaani upuuzi wa Rais dhalili wa Marekani — ambao umetolewa kwa nia ya kuiunga mkono serikali ya Kizayuni na kuchochea mifarakano baina ya nchi za Kiislamu — unazitaka serikali zote za eneo hili, kuupa kipaumbele mshikamano ndani ya ukanda huu na kuutazama kwa jicho la kipekee mgogoro wa Ghaza, zisiruhusu utekelezaji wa malengo ya kibeberu ya Marekani katika eneo hili.

Kituo cha Usimamizi wa Hawza

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha