Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kikundi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjat-ul-Islam Sayyid Shahwar Naqvi Amrohwi katika hotuba yake katika Msikiti Mkuu wa Shia Mirza Quli Khan, alisisitiza kuhusu ukubwa wa Qur'ani tukufu na kusema kwamba siri ya maendeleo na mafanikio ya binadamu iko katika kutekeleza mafundisho ya Qur'ani tukufu.
Alieleza kuhusu hadhi ya juu ya Qur'ani tukufu na jukumu lake la kuongoza, akisisitiza kwamba kitabu hiki cha mbinguni ni ufunguo wa furaha na maendeleo ya binadamu. Mwenyezi Mungu aliteremsha kitabu hiki kwa ajili ya kuongoza wanadamu na katika kitabu hiki kuna siri ya maendeleo ya binadamu. Qur'ani ni kitabu cha maisha na kimejaa suluhisho la masuala yote ya maisha, hata wafuasi wa dini nyingine wananufaika na kitabu hiki na kufikia malengo yao, ikiwa mafundisho ya Qur'ani yatapewa kipaumbele katika jamii, amani na utulivu Duniani kote vitaweza kudumu.
Hujjat-ul-Islam Shahwar Naqvi alisisitiza umuhimu wa kusoma Qur'ani kila siku, akisema: "Leo hii zaidi kuliko wakati mwingine wowote, kila mtu katika umma wa kiislamu anahitaji kujua mafundisho ya kitabu hiki na kuyatumia katika maisha yake, kusoma Qur'ani kunalete nuru na amani katika maisha ya mwanadamu, Qur'ani ni nuru, na nuru hakika itadhihirika katika maisha ya binadamu."
Maoni yako