Kwa mujibu wa Timu ya Tarjama ya Shirika la Habari la "Hawzat", Ayatollah Syed Mohammad Taqi Mudarrisi, mmoja wa Wanazuoni wa Iraq, alipotembelea ujumbe kutoka Yemen, alisisitiza kwamba kuongezeka kwa mashinikizo dhidi ya Taifa toka kwa mataifa, ni utangulizi wa faraja na ufunguzi unaokaribia kutokea kwenye upeo wa macho yetu, na akanukuu maneno ya Hadhrat Amirul-Muminin (amani iwe juu yake), kwamba alisema: "Faraja ya karibu mno kupatikana, ni pale mambo yanapokuwa magumu."
Aliongeza: Uongozi wa jamii unafanikiwa pale tu mamlaka zinapoangalia maslahi ya watu wote na kutotofautisha makundi na koo za watu.
Ayatollah Mudarrisi amefafanua: Kuangalia kutoka juu kunaondoa vikwazo na tofauti baina ya watu katika jamii na hivyo kuuwezesha uongozi kukabiliana na kila mtu kwa haki na bila ya ubaguzi, lakini ikiwa uongozi unatumia ubaguzi katika mtazamo wake kwa watu, na hautizami mtu mmoja mmoja, Uongozi huo hautayafikia matokeo na kamwe hautafanikiwi katika uongozi.
Mwanachuoni huyu wa Kiiraq alibainisha: Mitume, Mawalii, na Wanazuoni ndio mifano bora zaidi ya kuigwa katika uwanja huu, wakiwa na mtazamo mpana ambao unamweka kila mtu katika uwanja huo.
Akaendelea kusema: Vile vile tunaona kuwa Nabii wa Mwenyezi Mungu Musa (amani iwe juu yake) alimuomba Mola wake kukifungua kifua chake ili iwe rahisi kwake kuwaongoza wana wa Israeli, na pia kuhusu Mtume wa Uislamu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye Mwenyezi Mungu anamwaambia akisema:
أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ.
Je, hatukukunjulia kifua chako?
Akasema kwa kufafanua kuwa: "Kukunjua" huku ndiko kunakozikutanisha nyoyo na kuziunganisha juhudi za pamoja, vivyo hivyo, tunapowaelezea Wanachuoni wetu wema kuwa ni wavumilivu na wasamehevu, ni kwa sababu wana nyoyo na wanazipatanisha (nyoyo) na kuziunganisha nafsi za watu.
Maoni yako