Ijumaa 12 Septemba 2025 - 23:41
Njia ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni ni kutoa jibu thabiti

Hawzah / Khatibu wa Ijumaa wa Teheran amesema: Kama Imamu wa Ijumaa wa Teheran nasema, kwa serikali za Misri, Jodani, Bahrain na Saudi Arabia kwamba, iwapo Israeli itapata nguvu, itazishambulia pia nchi zenu, Kaulimbiu yake (Netanyahu), “Israeli Kubwa” — yaani kutoka Mto Nile hadi Mto Furat — inamaanisha anataka kupata sehemu za Misri na Jodani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Teheran, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami, Imamu wa muda wa mji mkuu, katika hotuba zake za swala ya ijumaa wiki hii iliyoswaliwa Chuo Kikuu cha Teheran, kwa kuashiria mipango ya Wiki ya Umoja na sherehe za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Imamu al-Sadiq (a.s.), alisema: Matukio mazuri yalifanyika nchini na hili linaonyesha kuwa Shi’a; wanafurahia pamoja na Ahlul-Bayt (a.s.) katika sherehe zao na wanahuzunika katika majonzi yao, wiki ya Umoja ni ubunifu wa Jamhuri ya Kiislamu lakini chanzo cha asili cha ubunifu huo ni Imamu al-Sadiq (a.s), Katika nchi yetu Shi’a na Sunni wanaishi pamoja bila matatizo.

Khatibu wa Ijumaa wa Teheran alipokuwa akizungumzia juu ya shambulio la hivi karibuni la Israeli dhidi ya Qatar na makao ya Hamas, alisema: Asili ya utawala huu wa Kizayuni ni kutafuta damu; ulizaliwa kwa kutumia damu miaka 80 iliyopita, na tarehe 25 Shahrivar mwaka huu ni kumbukumbu ya mauaji makali ya Palestina katika kambi ya Sabra na Shatila mwaka 1982, katika uhalifu huu Marekani hakika ilikuwa na mkono wake, na anga za Qatar ziko chini ya ulinzi wa kambi ya anga ya Al-Udeid ya Marekani — na ni vipi wasingepewa habari? Wengine wamesema ilikuwa muhimu Israeli kufanya hivyo, na Trump pia alisema anahuzunika — si kwa ajili ya kumpenda Qatar, bali kwa sababu walishindwa na wakuu wa Hamas walinusurika.

Ayatullah Khatami aliendelea kusrma: Wote wameitikia kitendo hiki cha Israeli, na baadhi ya nchi ambazo zilikuwa zikishindana kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israeli zimekataa uhalifu huu; kama Imamu wa Ijumaa wa Teheran nasema, kwa serikali za Misri, Jodani, Bahrain na Saudi Arabia, iwapo mtenda uhalifu huyu wa kikatili atapata nguvu, atawaushambulia nanyi pia, kaulimbiu yake (Netanyahu), “Israeli Kubwa”, inamaanisha kutoka Nile hadi Furat na anataka kuchukua sehemu za Misri na Jodani.

Alieleza kuwa: Njia ya kukabiliana na Israeli si kwa kuomba Umoja wa Mataifa au kutegemea taasisi za kimataifa; anashambulia mbele ya macho ya ulimwengu, njia pekee ni kuiondosha Israeli, lazima tukusanye nguvu zetu zote na kuminyana na utawala wa Kizayuni, Imamu Ali (a.s.) katika Nahj al-Balagha alisema: “Jibu kwa mtupaji mawe ni kwa kutumia jiwe,” Kuanzia mwanzo, wasuluhishi wa dunia ya Kiislamu walisema uvimbe huu wa saratani unapaswa kuondolewa, na Imamu wa Mapinduzi alisema utawala huu unapaswa kufutwa kwenye uwanja wa dunia; na angalau hatua ya msingi ni kwamba nchi za Kiislamu zikate uhusiano wa kisiasa na kiuchumi na utawala huu wa kikatili.

Imamu wa muda wa Ijumaa wa Teheran alisema: Msafara wa uvumilivu ni wa kupongezwa, ukijumuisha meli zaidi ya 70 kutoka nchi 44 za dunia pamoja na ushiriki wa mamia ya wanaharakati wa kimataifa — huu ni umoja uliopitiliza ambao unastahili pongezi.

Ayatullah Khatami aliongeza: Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Kiarabu walirudia tena kauli zao za zamani; na ninawaambia; visiwa vitatu ni mali ya Iran na vitabaki hivyo; maneno hayo ni mchezo wa Israeli na Marekani, Israeli inazungumza kuhusu “Israeli Kubwa” na inataka kuzipora nchi hizo, wote wajue Iran si adui wa yeyote katika majirani zake, lakini hatutaruhusu akaiba ardhi yetu.

Alisema kuwa: Kuinyang'anya silaha Hezbullah ni hatari sana; si kwa ajili ya Lebanon pekee bali kwa ajili ya dunia ya Kiislamu. Hezbullah ya Lebanon inapaswa kuvunja jino la yule mwendawazimu wa utawala wa Kizayuni ambaye ameweka meno kali, ninaishauri serikali ya Lebanon kwamba; ipo katika kosa kubwa — Hezbullah ni mkono wenye nguvu wa Lebanon, na wautegemee mkono huo.

Maoni yako

You are replying to: .
captcha