Ijumaa 29 Agosti 2025 - 00:26
Moqtada Sadr: Kuchomwa Qur’ani Tukufu na mgombea ubunge wa Marekani ni uhalifu wa kimataifa usiosameheka

Hawza/ Sayyid Moqtada Sadr, kiongozi wa Harakati ya Kitaifa ya Kishia nchini Iraq, amesisitiza kwamba kitendo cha kuchomwa Qur’ani Tukufu kilichofanywa na mgombea ubunge wa Marekani ni uhalifu wa kimataifa usiosameheka

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Moqtada Sadr leo Jumatano alisema kwamba kuchoma Qur’ani Tukufu na mgombea Myahudi wa bunge la Marekani, ambaye ni mhalifu, kumeonesha wazi udhaifu na ufisadi (wa “nyani na nguruwe”), na kwa mara nyingine Magharibi imeonesha meno yake ya sumu na kutangaza chuki yake dhidi ya dini ya Mwenyezi Mungu, Uislamu.

Aliongeza: “Hili halishangazi, lakini la kushangaza ni ukimya wa wenzetu wa kidini wanaopenda dini za mbinguni, mbele ya tendo hili la kihalifu na la aibu linalochochea chuki na kushambulia hisia na imani za mamilioni ya watu, ukimya huu unatokana tu na kuachana na (cheo cha juu cha kiroho).”

Moqtada Sadr aliendelea: “Isipokuwa hivyo, hili litabakia kuwa uhalifu wa kimataifa usiosameheka ambao utatikisa vyombo vya habari na taasisi zisizo za kibinadamu, Je, kukubali dini si sehemu ya uhuru? Na je, kushambulia dini si aina ya kukandamiza uhuru wa dini na imani?”

Akaongeza tena: “Lakini Mwenyezi Mungu amefichua uongo wa uhuru wenu na demokrasia yenu isiyo na heshima mnayoitumia kwa mizani ya upendeleo, lolote lililo dhidi yenu ni haramu na marufuku, na lolote lililo dhidi ya maadui zenu ni halali, lolote linalowafaidisha ni wajibu, na lolote linalowafaidisha wale mnaowapinga ni ugaidi, udikteta na kurudi nyuma.”

Mwishowe, Moqtada Sadr alisema: “Enyi mlio nyuma kimaendeleo, iwapo adhabu ya mbinguni itakufikieni, ngao zenu za chuma na silaha zenu hazitawasaidia, basi subirini, nami pia nipo pamoja na nyinyi katika wale wanaosubiri.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha