Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Bwana Pedro Sánchez, Waziri Mkuu wa Uhispania, katika hotuba yake ya hivi karibuni sambamba na kutangaza mipango ya baadaye kwa ajili ya nchi hii alisema:
“Kile ambacho Wazayuni wanakifanya si kujilinda, wala si shambulio la kawaida; haya ni mauaji ya kimbari na ni maangamizi ya watu kwa namna ya kikatili zaidi, kitendo hiki ni uvunjaji wa sheria zote za kimataifa haya ni maafa.”
Akaongeza kwa kusema:
“Serikali ya Uhispania, mbali na kuwa imekuwa ikitekeleza kwa dhati tangu Oktoba 2023 sheria ya kuiwekea Israel marufuku ya uuzaji wa silaha, pia imepiga marufuku meli za mafuta za kuelekea Israel kupita katika bandari zake, aidha, tunakusudia hadi mwishoni wa mwaka 2026 kutoa zaidi ya euro milioni 150 kwa ajili ya misaada ya kimsingi na kibinadamu kwa watu wanyonge wa Ghaza, mimi ninatarajia Bunge la Uhispania lipitishe suala hili.”
Miongoni mwa hatua nyingine za Waspania ni kuwekea vikwazo bidhaa zinazozalishwa na Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, na pia kutangaza kuwa yeyote aliyeshiriki moja kwa moja au kuhudumu katika mauaji ya kimbari ya Ghaza atapigwa marufuku kuingia Uhispania.
Hata hivyo, tunaelewa kuwa hatua hizi hazitoshi kwa ajili ya kutatua mgogoro mgumu ulioko Ghaza, lakini Serikali ya Uhispania siku zote imekuwa mkosoaji wa wazi wa vita vya Ghaza, na tunatarajia kwamba hatua zetu za kumlazimisha Netanyahu ziwe za kutosha, Israel tangu mwanzo wa vita vyake vipya dhidi ya watu wa Ghaza imewaua zaidi ya watu 64,000.”
Chanzo: Yahoo News
Maoni yako