Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, mashabiki wa timu ya taifa ya Italia mara nyingine tena waligeuza nyuso zao na kugeukia nyuma wakati wimbo wa utawala wa Kizayuni unapigwa, timu ya Italia inashiriki katika michezo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 katika kundi hili.
Tukio kama hili lilitokea pia mwaka 2024 wakati timu hizi mbili zilipokutana.
Aidha, barua rasmi kutoka Chama cha Makocha wa Michezo cha Italia imetumwa ikiitaka UEFA na FIFA kuiondoa na kuisimamisha timu ya Israel katika mashindano ya kimataifa ya michezo kutokana na jinai za kibinadamu ambazo utawala huo bandia umekuwa ukizifanya huko Ghaza na Palestina.
Chanzo: Football Italia
Maoni yako