Jumatano 10 Septemba 2025 - 21:39
Umoja wa Kiislamu ni Wajibu wa Kisheria na Silaha ya Muqawama, ni Rasilimali ya Uislamu Wote

Hawza/ Katibu Mkuu wa Harakati ya Ummah ya Lebanon, akisisitiza kuwa umoja wa Kiislamu si chaguo la hiari bali ni jukumu la kisheria, alisema: “Silaha ya muqawama huko Palestina, Lebanon na Yemen si mali ya kundi fulani pekee, bali ni rasilimali ya umma mzima wa Kiislamu, na hakuna yeyote mwenye haki ya kuinyang’anya kutoka kwa mataifa.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Shaykh Abdullah Jabri, Katibu Mkuu wa Harakati ya Ummah Lebanon, katika mahojiano na mwandishi wa habari wa shirika la habari la Hawza huko Mashhad, akitoa pongezi kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w) na wiki ya umoja, alisema kuwa kufungamana kwa matukio hayo ni fursa muhimu ya kuusoma upya ujumbe halisi wa Uislamu na kuimarisha mshikamano wa umma wa Kiislamu.

Akiashiria kuwa mwaka huu sherehe hizo zimeambatana na kumbukumbu ya miaka elfu moja na mia tano tangu kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), aliongeza kuwa: “Baadhi wanaweza kuona umoja wa Kiislamu kama jambo la hiari, lakini Qur’ani Tukufu kwa amri yake ya wazi:


 «وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِیعًا وَلَا تَفَرَّقُوا»

Shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakane

imeufanya umoja huu kuwa ni jukumu kwa Waislamu wote.”

Shaykh Jabri akakumbushia msimamo wa Imam Khomeini (r.a) kuhusu kusisitiza mshikamano wa umma, akasema: “Mtume Mtukufu (s.a.w.w) aliulinganisha umma na mwili mmoja; iwapo kiungo kimoja kitaumia, viungo vingine husononeka kwa homa. Leo hii ambapo umma wa Kiislamu uko chini ya mashambulizi ya pande zote, mshikamano ni wa dharura zaidi kuliko wakati wowote.”

Vitisho vya Kimataifa na Ulazima wa Ushirikiano wa Kivitendo

Akiashiria juhudi za vyombo vya habari na baadhi ya mfumo ya kisiasa katika kudhoofisha muqawama, alisema: “Vichwa vya habari vinavyozungumzia kuondoa silaha za muqawama huko Palestina, Lebanon au sehemu nyingine za ulimwengu wa Kiislamu, kwa hakika ni jitihada za kukataa wajibu wa jihad – hali ya kuwa wajibu huu umekubaliwa na madhehebu yote ya Kiislamu na si mali ya kikundi fulani pekee.”

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ummah ya Lebanon alilaani miradi ya kuleta mgawanyiko chini ya vyeo kama vile “Dini za Ibrahimu” na njia za uvamizi wa kimaadili na kiutamaduni. Akaongeza: “Tunapodhalilishwa katika mambo yetu matukufu na shakhsia zetu za kidini, umma wote unawajibika kujibu, tofauti za madhehebu ya Kiislamu si tishio bali ni neema ya Mwenyezi Mungu, lakini kugawanywa na kuimarishwa kwa mipasuko ni janga linalopaswa kutokomezwa.”

Akaonya pia juu ya kuenea kwa maovu ya kimaadili kama vile uenezi wa upotovu wa kijinsia, kubadili jinsia na kupotosha utambulisho wa mwanadamu, akivitaja kama sehemu ya vita laini dhidi ya misingi ya umma wa Kiislamu, alibainisha: “Lengo la maadui ni kugawanya ardhi zetu na kuendesha miradi kama vile ‘Israel Kubwa’ ambayo hufichua asili halisi ya mipango ya Kizayuni.”

Silaha za Muqawama na Rasilimali za Umma: Amana ya Waislamu

Shaykh Jabri, akisisitiza juu ya nafasi ya msingi ya silaha za muqawama, iwe Palestina, Lebanon au Yemen, alisema: “Silaha hizi ni mali ya umma wote, na haziwezi kunyang’anywa kutoka kwa mataifa, ni chombo cha kujilinda kinachomilikiwa na madhehebu yote ya Kiislamu, na mbele ya dhulma za maadui, ndicho kinachohakikisha usalama na heshima ya Waislamu.”

Mwanafikra huyu wa Ahlus-Sunna, akisisitiza umuhimu wa rasilimali za kimkakati zikiwemo mafuta na gesi, alisema kuwa: “Utajiri huu ni rasilimali ya pamoja ya umma wa Kiislamu, na lazima ulindwe kwa mshikamano na mshikikano dhidi ya mipango ya Kiamerika-Kizayuni.”

Akahitimisha kwa kusema: “Maadui, kwa kushambulia rasilimali, muqawama na utambulisho wa umma wa Kiislamu, wanalenga kutawala mustakabali wa mataifa yote ya Kiislamu, njia pekee ya kuyakabili mafunzo haya ni kushikamana kivitendo na mshirikiano wa kina wa Waislamu wote.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha