Alhamisi 11 Septemba 2025 - 14:10
Kile kinachoifanya hawza kuwa mahsusi ni “ufikishaji ulio wazi” / Mjadala wa Mapinduzi ya Kiislamu ndiyo mjadala wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)

Hawza/ Mkurugenzi wa hawza za kielimu, katika sherehe ya ufunguzi wa mwaka mpya wa masomo ya kituo cha kielimu na utafiti cha tablighi alisema: tablighi ni “roho ya undani” ya shughuli zote. Sisi hatufanyi kazi za kielimu na utafiti kwa ajili ya pumbao au kwa ajili ya kugundua nukta ya kielimu pekee; kama ingekuwa hivyo, vyuo vikuu pia vinafanya hivyo, kile kinachoifanya hawza kuwa mahsusi ni “ufikishaji ulio wazi.”

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayetullah Alireza A‘rafi, mkurugenzi wa hawza za kielimu nchini, katika sherehe ya ufunguzi wa mwaka mpya wa masomo ya kituo cha kielimu na utafiti cha tablighi, sambamba na kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu wa Uislamu (saww) na Imam Sadiq (a.s), wiki ya umoja na mwanzo wa mwaka wa masomo katika elimu ya malezi, vyuo vikuu na hawza alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu katika ulimwengu wa malakut na mulk ana bendera iliyoinuliwa, na nuru yake ya mwangaza inang’aa katika ghaibu na shahada. Kwa mujibu wa riwaya na mijadala ya elimu za Kiislamu, Mtume wa Uislamu ni ṣādir awwal, kiumbe wa mwanzo, kiumbe bora zaidi katika ulimwengu mzima na kiumbe aliye karibu zaidi na dhati isiyo na mwisho ya Mwenyezi Mungu. Hali hii haipatikani mahali pengine popote. Baada ya daraja ya Uungu na Uumbaji, daraja la kwanza ni lile la unabii na haqiqat Muhammadiya, katika mlolongo wa daraja za mwanadamu mkamilifu, nafasi ya kwanza ni ya Mtume Mtukufu (saww).

Akaendelea kusema: Hadhi hizi za ghaibu na za undani mara nyingi zimezungumziwa katika vyanzo mbalimbali. Hususan katika irfaan ya Kiislamu, sehemu na vipengele vigumu na vikubwa vya shakhsia ya Mtume (saww) vimechorwa, hii ndiyo hadhi ambayo Qur’an imesema kumhusu: “Hakika wewe uko juu ya tabia tukufu” au “Hakika tumekutuma wewe kuwa shahidi, mbashiri na muonyaji.” Pia katika aya: “Naapa kwa mji huu, na hali ya kuwa wewe uko huru ndani ya mji huu,” iwe “lā” ni ya ziada au ni ya kukanusha, katika hali zote inaonesha ukubwa wa Mtume (saww). Ikiwa ni ya ziada, maana yake ni kwamba nnapa kwa Makkah ni kwa ajili ya kuwepo kwako wewe mwenye baraka, na ikiwa ni ya kukanusha, maana yake ni kuwa mradi wewe umo katika ardhi hii, siapi kwa kitu kingine chochote, Kwa hali yoyote, nuru ya kuwepo kwa Mtume ndiyo iliyoifanya Makkah na Ka‘bah kustahiki kuapwa.

Ayetullah A‘rafi akarejelea kuelezwa kwa sura tukufu ya Mtume (saww) katika aya za Qur’an Tukufu, riwaya na sehemu za Nahjul-Balagha na kusema: Mimi nina kumbukumbu za zamani ambazo nimekusanya yaliyokuja katika Nahjul-Balagha na riwaya kuhusu mtindo wa maisha wa Mtume katika nyanja za kibinafsi, kifamilia na kijamii; kuna zaidi ya nukta mia mbili mahsusi kuhusu Mtume (saww) zilizorekodiwa katika historia, hali ikiwa kwamba wakati wake vyombo vya habari na uandishi havikuwa vimeenea, kumbuka kuwa Mtume (saww) baada ya vita vya Badr alifanya sharti la kuwaachia huru baadhi ya mateka ni kuwafundisha watu kumi kusoma na kuandika, hii inaonesha jinsi gani sokoni mwa elimu na maarifa katika Jaziratul-‘Arab kulivyokuwa kame.

Akaongeza: Pamoja na hali hizo, sehemu kubwa ya ripoti za maisha ya Mtume (saw) zinahusiana na kipindi cha Madina, kipindi hiki kifupi lakini chenye matunda, ndicho kilichoacha athari kubwa zaidi ya sira ya Mtume katika historia na kikawa na taathira kubwa sana kwa tablighi ya dini, Mtume wa Uislamu tangu mwanzo aliweka ramani kuu ya njia ya kuokoa wanadamu na kufikisha ujumbe wake, tazama wakati huo hapakuwa na nyenzo za tablighi za leo, wala vyombo vya habari vya karne zilizofuata, katika ardhi kame isiyo na dola na ustaarabu, Mtume aliwezaje kufanya ujumbe wake uwe wa ulimwengu mzima?

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha