Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah A'rafi, akiendelea na ziara yake nchini Iraq, alifika katika nyumba ya Marehemu Ayatullah al-Udhma Sheikh Is'haq Fayyadh, mmoja wa Marajii Wakuu wa Taqlidi nchini Iraq, na kwa kusoma Suratul Fatiha alitoa heshima kwa hadhi tukufu ya Marjaiyya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya hapo Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, alizungumza na Hujjatul Islam wal-Muslimin Mahmoud Fayyadh, mtoto mkubwa wa marehemu Marjii huyo. Katika mazungumzo hayo alitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo chake na kukumbusha baadhi ya kumbukumbu zinazomhusu marehemu huyo.
Aidha, alielezea hadhi yake ya kielimu, akazungumzia darsa zake za Bahth al-Kharij, na akaeleza kwa ufupi baadhi ya huduma zake za kijamii alizozitoa katika kipindi chote cha maisha yake.
Mwishoni mwa ziara hiyo, Mkurugenzi wa Hawza alifika kwenye kaburi la Marjii huyo mkubwa, ambaye kwa mujibu wa wasia wake amezikwa katika nyumba yake, ambapo kwa pamoja walimsomea Suratul Fatiha.
Maoni yako