Jumamosi 18 Julai 2026 - 18:50
Kuwaamini madhalimu kunapingana na mafundisho ya Uislamu/ Marekani ndio chanzo cha utawala wa mabavu na uporaji wa mataifa

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mir Hussein Ziai amesema kuwa; kuwaamini madhalimu kunapingana na mafundisho ya Uislamu, ameitaja Marekani kuwa ndiyo chanzo cha utawala wa mabavu na uporaji wa rasilimali za mataifa, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha umoja wa Umma wa Kiislamu na kuendeleza uadilifu wa kijamii.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mir Hussein Ziai, msimamizi wa Chuo cha Elimu ya Dini cha Ahlul-Bayt (as) katika mji wa Sheberghan, Mkoa wa Jawzjan nchini Afghanistan, katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya Sheberghan zilizohudhuriwa na idadi kubwa ya waumini, wanafunzi wa vyuo na makundi mbalimbali ya wananchi, alisisitiza umuhimu wa kuimarisha umoja wa Umma wa Kiislamu, kupambana na ubaguzi na kueneza uadilifu wa kijamii.

Akieleza kuwa dhulma, ujinga na hofu ni miongoni mwa vikwazo vikubwa vinavyozuia maendeleo na ustawi wa mtu binafsi na jamii, alisema: Dhulma katika ngazi yoyote ile, kuanzia ndani ya familia hadi katika jamii, humzuia mwanadamu kufikia ukamilifu na maendeleo, na huwa sababu ya kuenea kwa matatizo mbalimbali ya kijamii.

Msimamizi wa Chuo cha Elimu ya Dini cha Ahlul-Bayt (as) katika mji wa Sheberghan, Mkoa wa Jawzjan nchini Afghanistan, akisisitiza mafundisho ya Kiislamu kuhusu kupambana na dhulma, alisema: Waislamu hawapaswi kusimama upande wa madhalimu, kuwaunga mkono au kuwaamini, kwani kushirikiana na dhalimu ni kushiriki katika dhulma na kukosekana kwa uadilifu.

Shahidi Balkhi; mbeba bendera ya umoja na mwamko wa Kiislamu

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ziai aliendelea na hotuba yake kwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 58 ya shahada ya Allama Sayyid Ismail Balkhi, akimtaja mwanazuoni huyo mashuhuri kuwa ni alama ya utambulisho, mwamko na uhai wa fikra za jamii ya Kiislamu.

Aliongeza kuwa; Shahidi Balkhi, kwa kutegemea mafundisho ya Tawhidi, aliweka mbele mapambano dhidi ya ukabila, mifarakano na taassubu za kikabila, huku akiuona umoja wa Umma wa Kiislamu kuwa ndiyo njia muhimu zaidi ya kukabiliana na migawanyiko na kufanikisha heshima na izza ya Waislamu.

Kukosoa sera za Marekani

Msimamizi wa Chuo cha Elimu ya Dini cha Ahlul-Bayt (as) katika mji wa Sheberghan, Mkoa wa Jawzjan nchini Afghanistan, katika sehemu nyingine ya hotuba yake alikosoa sera za Marekani na kueleza kuwa nchi hiyo ndiyo chanzo cha utawala wa mabavu na uporaji wa rasilimali za mataifa.

Alisema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, chini ya uongozi na maelekezo ya Ayatullah Khamenei, imefanikiwa kubainisha na kuufichua ukweli wa sera za Marekani mbele ya maoni ya umma wa dunia, na kuimarisha fikra ya kujitegemea, Muqawama na kupambana na ubeberu miongoni mwa mataifa huru.

Mwishoni mwa hotuba yake, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ziai alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi umoja, kueneza uadilifu, kupambana na ubaguzi na kushikamana na maadili ya Kiislamu, hukubakieleza kuwa hiyo ndiyo njia muhimu zaidi ya maendeleo na utukufu wa Umma wa Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha