Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, mmoja wa wanachama wa Harakati ya Kusini mwa Yemen (Al-Harak al-Janubi), ambaye pia ni mshiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Mazungumzo (miongoni mwa waliotia saini Mkataba wa Amani na Ushirikiano), amelaani shambulio la Saudi Arabia dhidi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sana'a na kulielezea kuwa ni uhalifu kamili wa kivita.
Harakati hiyo, katika taarifa yake, ilisema kuwa; uhalifu huo ni nyongeza nyingine katika rekodi ya uhalifu na umwagaji damu wa Saudi Arabia dhidi ya ardhi na wananchi wa Yemen.
Aidha, taarifa hiyo ilipongeza operesheni maalumu ya Jeshi la Yemen ya kulenga Uwanja wa Ndege wa Abha kama jibu la shambulio dhidi ya Uwanja wa Ndege wa Sana'a. Ilisisitiza kuwa Yemen haitakaa kimya mbele ya uchokozi wowote, hatua za kuongeza mvutano au vitendo vya kipuuzi vinavyofanywa na vikosi vinavyoishambulia, kuizingira na kuikalia nchi hiyo.
Katika taarifa hiyo pia, Saudi Arabia ilibebeshwa jukumu la kuvunjika na kusambaratika kwa mchakato wa kupunguza mvutano. Harakati hiyo ilitoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mjumbe wake maalumu kutekeleza wajibu wao kuhusu suala hilo.
Mwishoni mwa taarifa hiyo, harakati hiyo ilitoa pongezi kwa nafasi na msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kusimama pamoja na wananchi wa Yemen na kusaidia juhudi za kuvunja mzingiro dhidi ya nchi hiyo.
Maoni yako