Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, marufuku na waraka zinazotolewa na Idara ya Wakfu wa Ja'fari nchini Bahrain hazimdanganyi tena hata Muislamu mmoja wa Kishia wa nchini humo. Kimsingi, waraka hizo hazikuwahi kuwa za kuaminika tangu mwanzo, na baada ya muda imethibitisha kwamba hakuna hata uamuzi mmoja wa taasisi hiyo unaolenga maslahi ya wafuasi wa madhehebu hayo, bali yote hutolewa kwa ajili ya kulinda maslahi ya utawala.
Kabla ya kuanza kwa siku za maombolezo ya mwezi wa Muharram, serikali ilitoa rahadharu nyingi katika mfumo wa vita dhidi ya jamii ya Kishia, zikielekezwa hasa kwenye shughuli za maombolezo ya Imam Hussein (as) katika mwezi wa Muharram. Chombo kilichotumiwa kutekeleza matakwa ya utawala kilikuwa ni Idara ya Wakfu wa Ja'fari, ambayo, kama ilivyotarajiwa, haikuonesha hatua yoyote ya kuzuia mashambulizi makali dhidi ya utambulisho wa Kishia nchini humo pamoja na dhidi ya alama zao, taasisi zao, wanazuoni wao na waombolezaji wao.
Licha ya vitisho vyote, vitendo vya kutisha wananchi na kukamatwa kwa watu mbalimbali, msimu wa maombolezo ulifanikiwa kwa kiwango kikubwa, na mafanikio hayo yalitokana na juhudi za wananchi wenyewe. Hata hivyo, simulizi halikuishia hapo. Serikali pamoja na vyombo vyake vya usalama viliendelea na sera ya kuzingira shaairi za Hussein, na kwa mara nyingine zikazitaka Husseiniyyah zisiache "kutii" mamlaka hizo na zifuate masharti yaliyowekwa, kama vile kufanya maombolezo ndani ya Husseiniyyah pekee na kutotumia vipaza sauti vya nje.
Ni nini kilitokea? Husseiniyyah zilichukua msimamo wa muhimu mbele ya uingiliaji huu wa wazi katika ibada za kidini za Hussein (as). Zilipinga uamuzi wa taasisi rasmi uliokataza maandamano ya maombolezo katika siku ya shahada ya Imam Zaynul Abidin (as), pamoja na kuamuru kuzimwa kwa vipaza sauti vya nje wakati wa hotuba na maombolezo.
Idadi kubwa ya Husseiniyyah ziliamua kufuta sehemu ya kawaida ya shughuli za maombolezo kama ishara ya kupinga uamuzi wa serikali wa kuzuia maandamano ya maombolezo kupita barabarani. Hii ilikuwa hatua ya wazi ya kuinyonga shughuli hiyo na kuweka udhibiti kamili kwa kuizuia ibakie ndani ya majengo na kumbi pekee. Msimamo huu hauwezi kutafsiriwa kuwa ni kitu kingine isipokuwa ni kilio cha wazi dhidi ya uingiliaji wa serikali katika masuala ya Waislamu wa Kishia na katika ibada za Hussein, hasa baada ya uingiliaji huo kufikia kiwango kisichovumilika.
Maoni yako