Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika hotuba za Swala ya Ijumaa alizozitoa katika Husseiniyyah A'dham Fatimiyyah mjini Najaf Ashraf, alitoa salamu za pole kwa familia za mashahidi miongoni mwa mazuwari wa Imam Hussein (as) kutoka mji mtukufu wa Basra waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani walipokuwa njiani kuelekea ziarani.
Aliongeza: "Sambamba na kutoa pole kwa familia zao, ndugu zao na wananchi wetu wote wapendwa wa Basra, tunawapongeza kwa fadhila ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewajalia, kuhusiana na hilo, nitawasomeeni riwaya tukufu zilizopokewa:
Hisham bin Salim amepokea kwamba alimuuliza Imam Swa'diq (as): 'Je! Ni thawabu gani anayopata mtu anayefariki akiwa safarini kuelekea kwa Imam Hussein (as)?'
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf aliendelea kusema kwamba Imam Sadiq (as) alijibu:
"Malaika humsindikiza, humletea kutoka Peponi manukato ya kuoshea maiti na mavazi, anapovishwa sanda humswalia, kisha humfunika kwa sanda nyingine juu ya sanda yake, hhini ya miguu yake hutandazwa mimea yenye harufu nzuri, na ardhi hupasuliwa kwa namna ambayo mbele yake, nyuma yake, kuliani na kushotoni kwake hujaa nuru na utukufu, mlango kutoka Peponi hufunguliwa kuelekea kaburini kwake, na harufu nzuri pamoja na neema zake humfikia hadi Siku ya Kiyama."
Na katika riwaya nyingine kutoka kwa Abu Sa'id al-Qadhi imepokewa kwamba, alisema:
"Niliingia kwa Imam Swa'diq (as) nikamsikia akisema: 'Yeyote anayekwenda kwa miguu kuzuru kaburi la Imam Hussein (as), Mwenyezi Mungu humwandikia kwa kila hatua anayopiga thawabu ya kumkomboa mtumwa mmoja katika kizazi cha Ismail.'
Kisha Imam (as) akaongeza: "Na yeyote anayemjia kwa njia ya bahari, Mwenyezi Mungu huwapa utulivu waliomo ndani ya chombo hicho, na mnadi kutoka mbinguni hulingana: 'Mmekuwa watoharifu, na Pepo imeandaliwa kwenu ikiwa safi na yenye kupendeza.'"
Basi, hongera kwa mazuwari hawa waliokuwa wakielekea kwa Imam Hussein (as); hongera kwa familia zao na kwa wananchi wetu wapendwa wa Basra.
Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, akizungumzia masuala ya ndani ya Iraq, alisema: "Watu wote wamefurahishwa na kufichuliwa kwa mafaili ya ufisadi pamoja na kiwango kikubwa cha fedha kilichohusika katika faili la 'Sawlat al-Fajr'. Hapa tunatoa mapendekezo matatu: kwanza, suala hili lisihusishwe na siasa; pili, lisitumike kwa misingi ya madhehebu; na tatu, lihifadhiwe mbali na shinikizo za ndani na za nje."
Aliongeza: "Tunaitaka Serikali ya eneo la Kurdistan isiruhusu makundi ya wapinzani wa mapinduzi kufanya uvamizi na mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na izuie kufunguliwa kwa makao na kambi zao huko Erbil na maeneo mengine. Iran imetangaza kwamba baada ya kushambuliwa kwa madaraja na bandari zake, itayalenga madaraja na bandari za Bahrain, Kuwait, Saudi Arabia, Qatar, Falme za Kiarabu na Jordan, na hiyo ni haki yao."
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf alihoji: "Je, tunataka jambo kama hilo litokee pia Iraq na nchi hii iwe sehemu ya kuanzia mashambulizi? Sisi tuko pamoja na Jamhuri ya Kiislamu; tuna hatima moja, na maisha bila wao hayana kheri wala maslahi."
Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi, akizungumzia masuala ya kimataifa, alisema: "Kuhusu ziara ya Waziri Mkuu kwenda Marekani, tunasisitiza kwamba mafanikio ya kiuchumi yasije yakapatikana kwa gharama ya mamlaka, uhuru na mahusiano ya kisiasa ya Iraq, wala kwa gharama ya hisia za wananchi wetu, kujitolea kwao na damu ya mashahidi wetu."
Aliendelea kusema: "Tunasikitishwa na kauli za Rais wa Marekani ambazo zinapingana na hisia za taifa letu pamoja na maadili ya jihadi na kujitolea mhanga ya wananchi wetu."
Imamu wa Sala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf alisema: "Tunaamini kwamba taifa la Iraq tayari limemjibu Rais wa Marekani kuhusu suala la kuuawa kishahidi Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis. Ushiriki wa Wairaq milioni katika mazishi ya Imam Shahidi Khamenei uliudhihirishia ulimwengu jinsi Wairaq wanavyomtazama muuaji, na hilo ndilo jibu lenyewe."
Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanchi katika sehemu nyingine ya hotuba yake alisema: "Katika kivuli cha vita kati ya Iran na Marekani, tunasisitiza kwamba anga na ardhi ya Iraq havipaswi kutumiwa kama njia ya kufanya mashambulizi dhidi ya Iran au nchi nyingine yoyote, endapo jambo hilo litatokea, huenda tukakabiliwa na matokeo yasiyopendeza."
Maoni yako