Jumapili 19 Julai 2026 - 00:26
Taifa la Iran Lina Mafunzo Yasiyosahaulika kwa Adui wa Marekani

Hawza/ Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Uvunjaji wa makubaliano kwa mara nyingine umethibitisha kutokuwa na thamani na kutokuwa na uhalali wa saini ya Rais wa Marekani."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu hamasa kubwa katika mazishi ya Bwana Shahidi wa Iran na ufafanuzi wa masuala muhimu ya nchi umechapishwa.

Ujumbe wa Ayatullah al-Udhma Imam Sayyid Mujtaba Khamenei ni kama ifuatavyo:

Sambamba na hamasa hii [ya kuandamana katika mazishi ya Bwana Shahidi wa Iran], uvunjaji wa ahadi mara kwa mara uliofanywa na Shetani Mkuu kuhusu makubaliano yaliyotiwa saini kati ya marais wa Iran na Marekani, kwa mara nyingine umethibitisha kwa kila mtu ukweli wa kwamba saini ya Rais wa Marekani haina thamani wala uhalali wowote, na kwamba uonevu, kutaka kutawala kila kitu, na unyama ni sehemu zisizotenganishwa za mwenendo na misingi ya Marekani.

Leo hii, Shetani Mkuu kwa mara nyingine ameufichua uso wake halisi bila pazia, ili tajriba hii yenye giza ya uhalifu na kuvunja ahadi iwe ushahidi mwingine madhubuti wa uongo, kutokuwa na mantiki, kutokuwa wa kuaminika na uchafu wa Marekani.

Sasa kwa kuwa adui Mmarekani anatafuta kuchochea vita na kubeba gharama nzito zaidi pamoja na fedheha kubwa zaidi, basi ajue kwamba; taifa pendwa la Iran na Mhimili wa Muqawama vina mafunzo yasiyoweza kusahaulika kwa ajili yake, ambayo ushujaa wa wapiganaji wa Uislamu na ari ya watu jasiri wa maeneo ya kusini katika siku hizi umeonesha baadhi ya mifano yake.

Miongoni mwa Mambo ya Msingi Zaidi ni Kusisitiza Umoja Mtakatifu katika Ngazi Zote,bKuepuka Mgawanyiko na Mivutano ni Wajibu wa Kila Mtu, Ni lazima niwaambie ninyi watu waaminifu na wenye heshima wa Iran, kwamba; miongoni mwa mambo ya msingi kabisa katika kipindi hiki ni kusisitiza kauli moja na umoja mtakatifu katika ngazi zote za wananchi na viongozi, na katika nyanja zote, kwa ajili ya kutimiza malengo ya juu ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuhakikisha heshima na uhuru wa Iran pendwa, hususan mbele ya adui mhalifu na mdanganyifu wa Marekani.

Kama ilivyosisitizwa mara nyingi hapo kabla, kulinda umoja na kujiepusha na mgawanyiko, mivutano, tofauti za kisiasa na kuzipa uzito tofauti za kijamii ni wajibu wa wote. Bila shaka, nafasi ya viongozi pamoja na watu wenye kujitolea na mapenzi ya dhati kwa Mapinduzi, Imam na Kiongozi Shahidi katika kudumisha mshikamano na umoja wa nchi ni muhimu zaidi na yenye hisia kubwa zaidi.

Kuwaamini Viongozi Kunahakikisha Ulinzi wa Maslahi ya Iran/ Kukosoa Utendaji wa Viongozi isiwe Sababu ya Kuwadhulumu Wasio na Hatia au Kuvunja Umoja wa Jamii

Taifa pendwa, kwa kuendelea kuwaamini viongozi wenye kujitolea katika mihimili yote mitatu ya dola, ambao juhudi zao kwa ajili ya ustawi na mafanikio ya taifa zinaonekana wazi, litaendelea kuwa makini na lenye kushiriki kikamilifu katika uwanja wa kulinda maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Huenda baadhi ya watu, kwa ikhlasi kamili na kwa nia njema, wakawa na ukosoaji kuhusu utendaji wa baadhi ya viongozi. Kwa mtazamo wangu, pamoja na kwamba kujali huku na wasiwasi wao kwa ajili ya mfumo wa Kiislamu ni mtaji mkubwa wenye thamani, na wenyewe ni jambo linalopendeza, watu hawa wema ambao baadhi yao ni miongoni mwa vinara wa uoni wa mbali wanapaswa kuwa waangalifu ili mwenendo huu:

Kwanza, usisababishe kumdhulumu mtu asiye na hatia, kwa kuwa jambo hilo lenyewe huwa chanzo cha kunyimwa baraka na neema za Mwenyezi Mungu.

Pili, usiwe sababu ya kuvunjika kwa umoja na mshikamano wa kijamii. Kwa kuzingatia mambo haya, ukosoaji utakuwa sababu ya maendeleo na ustawi wa mambo.

Adui hapaswi kupata ishara yoyote ya udhaifu kutoka kwetu, ikiwemo udhaifu huu. Endapo tutazingatia kwa ukamilifu tahadhari hizi, adui atalazimika kukimbia kwa kushindwa.

Mazishi ya Bwana Shahidi wa Iran Yalikuwa Hamasa ya Kihistoria na Mwamko Usio na Mfano

Enyi taifa kubwa na la ajabu la Iran!

Salaam, salamu na shukrani ziwe juu yenu, ambao kwa hamasa yenu ya kipekee na ya kihistoria katika mwamko usio na mfano wa kuandamana katika mazishi ya Bwana Shahidi wa Iran, mmeweka kiwango kipya cha kudhihirisha mwamko, azma thabiti ya utambulisho wa Kiislamu katika kuthamini uaminifu, utambuzi wa kina na kuonesha mapenzi makubwa kwa Kiongozi wa Umma wa Kiislamu na Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi.

Joto la nyoyo zilizowaka, macho yaliyolengwa na machozi, na azma thabiti ya mamilioni ya watu waliokusanyika katika misafara ya makumi ya kilomita huko Tehran, Qom, Mashhad na miji pamoja na vijiji vingine, limewafanya marafiki wa taifa la Iran na watu huru duniani kuwastaajabia, huku likiwaacha maadui wenye kiburi wa taifa la Iran katika mshangao, kuchanganyikiwa, hasira na hofu.

Shukrani kwa Taifa la Iran kwa Kuumba Hamasa Hii na kwa Juhudi za Marjaa na Wasomi katika Kuandamana kwenye Mazishi ya Bwana Shahidi wa Iran

Natoa shukrani zangu za dhati kwa kila mmoja wa wananchi wapendwa ambao wenyewe ni wafiwa wa baba shahidi wa Umma, na ambao licha ya ugumu, vikwazo na changamoto mbalimbali, walishiriki katika tukio kubwa la kuandamana katika mazishi ya Bwana Shahidi wa Iran na kuumba hamasa ya kihistoria.

Vilevile ninawashukuru Marajii watukufu wa Taqlid, wanazuoni, wasomi na wabobezi, wanaharakati wa masuala ya utamaduni, kijamii na kisiasa, pamoja na taasisi za kiraia na za kijeshi kwa hatua na juhudi zao. Aidha, ninathamini uwepo wa viongozi na wawakilishi wa Mhimili wa Muqawama wenye heshima na harakati tukufu za Kiislamu.

Ninatumaini kwamba wote walioshiriki, kwa namna yoyote ile, katika hamasa hii ya kihistoria kwa uwepo wao, ushirikiano wao na mshikamano wao, watapata uangalizi maalumu na dua ya bwana wetu, Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha