Jumatano 15 Julai 2026 - 11:35
Umoja na Kushikamana na Njia ya Imam Shahidi Ndio Dhamana ya Mustakabali Mwema wa Muqawama

Hawza/ Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, alasiri ya Jumatatu, 28 Muharram 1448 Hijria Qamaria, sawia na 13 Julai 2026, alihudhuria kongamano lililopewa anuani "Mustakabali wa Muqawama Baada ya shahada ya Imam Khamenei (qs)", lililoandaliwa na Kamati ya "Nidaa al-Wali" katika mji wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq, ambapo alitoa hotuba kwa washiriki.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, alasiri ya Jumatatu, 22 Tir 1405 Hijria Shamsia, alishiriki katika kongamano hilo lililopewa anuani "Mustakabali wa Muqawama Baada ya shahada ya Imam Khamenei (qs)", lililoandaliwa na Kamati ya "Nidaa al-Wali" jijini Baghdad, mji mkuu wa Iraq, na akawahutubia washiriki.

Katika hotuba yake, Sheikh Zakzaky alisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano miongoni mwa nguvu za Muqawama, huku akiwataka mujahidina na wanaharakati wa Mhimiili wa Muqawama kuendelea kwa uthabiti na subira katika njia na malengo ambayo Imam Shahidi alitoa maisha yake kwa ajili yake, na kuyaendeleza kwa nguvu na azma zaidi.

Kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria pia alizungumzia maendeleo yanayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwenguni, akisema kuwa, kuongezeka kwa mwamko na uelewa wa kizazi cha vijana ni miongoni mwa dalili zinazotoa matumaini makubwa kwa mustakabali wa Mhimiili wa Muqawama.

Aliongeza kuwa  mwenendo wa matukio ya sasa pamoja na mwitikio mkubwa wa vijana kwa malengo na maadili ya Muqawama ni bishara ya mustakabali wenye mwangaza kwa Muqawama duniani kote.

Kongamano la "Mustakabali wa Muqawama Baada ya shahada ya Imam Khamenei (qs)" lilihudhuriwa na idadi ya viongozi wa kitamaduni, wanazuoni wa dini na wanaharakati wa Mhimiili wa Muqawama jijini Baghdad, na lilijikita katika kujadili matarajio na mikakati ya kuendeleza fikra na mwelekeo wa Muqawama baada ya shahada wa Imam Khamenei (qs).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha